Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
Michuano ya robo fainali ya Kombe la Muungano 2026 imefikia tamati rasmi kufuatia kukamilika kwa mechi zote zilizokuwa zikiamua hatma ya timu kuelekea hatua inayofuata. Mchezo wa mwisho ulihusisha Simba SC dhidi ya Mafunzo FC, ambapo matokeo yake yamekamilisha orodha ya timu nne bora zilizofuzu. Sasa macho ya wadau wa soka yanaelekezwa kwenye hatua ya nusu fainali, inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vilivyofanikiwa kusonga mbele.
Hatua hii imezikutanisha baadhi ya timu zenye historia na ushindani mkubwa, hali inayoongeza hamasa kuelekea mechi zijazo za kuwania tiketi ya fainali.
Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Muungano Cup 2026
Baada ya michezo ya robo fainali, timu nne zimefanikiwa kusonga mbele na kuthibitisha ubabe wao ndani ya dimba la New Amaan Complex, Zanzibar:
- Simba SC – ilitinga nusu fainali kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Mafunzo FC
- Mlandege FC – iliiondoa Singida Black Stars kwa ushindi wa mabao 2-1
- Yanga SC – ilionesha ubora mkubwa kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Muembe Makumbi City
- Azam FC – iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ, mabao yote yakifungwa na Jean Ngita
Matokeo haya yameweka msingi wa mechi kali katika hatua inayofuata, huku kila timu ikiwa na lengo la kufika fainali.
Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
Ratiba rasmi ya mechi za nusu fainali imepangwa kama ifuatavyo:
Aprili 25, 2026 – Saa 2:15 Usiku
- Azam FC vs Yanga SC
Aprili 26, 2026 – Saa 2:15 Usiku
- Mlandege FC vs Simba SC
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply