Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya za Afya Zilizotangazwa July 2024

Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya za Afya Zilizotangazwa July 2024

Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa, ilitangaza nafasi za kazi 9483 katika fani mbalimbali za Afya tarehe 7 Julai 2024.

Nafasi hizi za kazi ni ishara ya juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya. Pia nafasi hizi za kazi zina lengo la kuboresha huduma za afya nchini, ambapo kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko ya huduma duni kwenye baadhi ya maeneo kutokana na upungufu wa wataalamu.

Serikali imejipanga kuboresha sekta ya afya kwa kuhakikisha kwamba vituo vya afya vinapata wataalamu wenye sifa na uwezo wa kutoa huduma bora kwa wananchi. Kama wewe ni muhitimu wa stashahada au shahada katika fani za Afya basi hii ni nafasi kwako ya kupata ajira serikalini na kutumia ujuzi wako kusaidia watu. Hapa tumekuletea taarifa kuhusu mwisho wa kutuma maombi ya ajira za afya julai 2024.

Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya za Afya Zilizotangazwa July 2024

Sifa za Waombaji Ajira Mpya Za Afya July 2024

  1. Waombaji wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
  2. Stashahada au Shahada: Waombaji wanatakiwa kuwa na stashahada au shahada kutoka katika taasisi zinazotambulika.
  3. Uzoefu: Uzoefu katika sekta ya afya utaongeza nafasi ya mwombaji kuchaguliwa.
  4. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  5. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal). Waombaji wanashauriwa kufuata hatua zifuatazo:

  1. Tembelea Tovuti Rasmi: Waombaji wanatakiwa kutembelea tovuti rasmi ya ajira kupitia anuani ifuatayo: portal.ajira.go.tz.
  2. Jisajili: Kama huna akaunti, ni muhimu kujisajili kwanza kwa kujaza taarifa muhimu.
  3. Ingia Kwenye Akaunti: Kwa wale ambao tayari wana akaunti, wanatakiwa kuingia kwa kutumia jina la mtumiaji na nenosiri.
  4. Jaza Fomu ya Maombi: Jaza fomu ya maombi kwa usahihi na hakikisha umeambatanisha vyeti vyote muhimu.
  5. Tuma Maombi: Baada ya kujaza fomu, hakikisha unakagua mara mbili kabla ya kutuma maombi yako.

Tarehe ya Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya za Afya

Mwisho wa kutuma maombi ya ajira za Afya zilizotangazwa na TAMISEMI siku ya julai 7 ni tarehe 20 Julai 2024. Ni muhimu kwa waombaji kuhakikisha kwamba wametuma maombi yao kabla ya tarehe hii ili kuepuka matatizo yoyote ya kiufundi au kuchelewa kwa maombi yao.

Soma Maelezo Zaidi Kuhusu Nafasi Hizi Za Ajira Kupitia

  1. Nafasi Mpya za Ajira Muuguzi II TAMISEMI 2024: Wauguzi 2282 Wahitaji
  2. Ajira za Afya Tanzania 2024: TAMISEMI Yatangaza Nafasi 9,000+!
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo