Orodha Kamili ya Makombe na Tuzo za Toni Kroos

Orodha Kamili ya Makombe na Tuzo za Toni Kroos

Mchezaji kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Toni Kroos, ametangaza kustafu rasmi baada ya Euro 2024, uku akiwa ameacha historia kubwa katika ulimwengu wa soka. Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 34, anayejulikana kwa upigaji pasi wake wa hali ya juu, akili ya mbinu, na idadi ya makombe ambayo amebeba, ametangaza kustaafu baada ya zaidi ya miaka 15 ya kucheza soka la ushindani.

Kustaafu kwa Kroos kumewashangaza mashabiki wengi, kwani wengi walitarajia angeendelea kwa angalau msimu mwingine.

Katika kipindi chote cha maisha yake ya soka, Kroos ametoa mchango mkubwa katika kila timu aliyochezea. Amekuwa mchezaji muhimu na mwenye ushawishi mkubwa, hasa akiwa katika kikosi cha Real Madrid, Bayern Munich, na timu ya taifa ya Ujerumani.

Uwezo wa kipekee wa Kroos uko katika ujuzi wake wa kupiga pasi za mwisho. Kross ni moja kati ya viungo ambao wamebadilisha kabisa nafasi ya kiungo wa ulinzi, kwa aina ya uchezaji wake wa kuongeza kasi ya mchezo kwa pasi zake sahihi na uwezo wa kuona mchezo. Utulivu wake katika kila mechi haswa mechi ngumu haukuwa wa kawaida, na kumruhusu kutuliza mchezo hata katika hali ngumu zaidi.

Orodha Kamili ya Makombe na Tuzo za Toni Kroos

Ubora wa Toni Kroos umewekwa wazi kupitia idadi kubwa ya makombe na tuzo ambazo amebeba akiwa na timu mbalimbali, ukidhihirisha ufanisi wake wa hali ya juu katika ulimwengu wa soka. Hapa kuna orodha kamili ya mafanikio yake

Orodha Kamili ya Makombe na Tuzo za Toni Kroos

Idadi ya Makombe ya Toni Kross

  1. Bundesliga: 2007–08, 2012–13, 2013–14
  2. DFB-Pokal: 2007–08, 2012–13, 2013–14
  3. DFL-Supercup: 2012
  4. UEFA Champions League: 2012–13
  5. UEFA Super Cup: 2013
  6. FIFA Club World Cup: 2013
  7. La Liga: 2016–17, 2019–20, 2021–22, 2023–24
  8. Copa del Rey: 2022–23
  9. Supercopa de España: 2017, 2019–20, 2021–22, 2023–24
  10. UEFA Champions League: 2015–16, 2016–17, 2017–18, 2021–22
  11. UEFA Super Cup: 2014, 2017, 2022
  12. FIFA Club World Cup: 2014, 2016, 2017, 2018, 2022
  13. FIFA World Cup: 2014

Idadi ya Tuzo Za Toni Kross

  1. UEFA European Under-17 Championship Golden Player: 2006
  2. UEFA European Under-17 Championship Top Scorer: 2007
  3. FIFA U-17 World Cup Golden Ball: 2007
  4. FIFA U-17 World Cup Bronze Shoe: 2007
  5. Fritz-Walter-Medal U18 Gold Medal: 2008
  6. kicker Bundesliga Team of the Season: 2009–10, 2011–12
  7. UEFA Champions League Squad of the Season: 2013–14, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2017–18
  8. FIFA FIFPro World11: 2014, 2016, 2017
  9. UEFA Team of the Year: 2014, 2016,
  10. IFFHS World’s Best Playmaker: 2014
  11. FIFA World Cup All-Star Team: 2014
  12. FIFA World Cup Dream Team: 2014
  13. Silbernes Lorbeerblatt: 2014
  14. German Player of the Year: 2014
  15. UEFA European Championship Team of the Tournament: 2016
  16. La Liga Top Assist Provider: 2016–17
  17. UEFA La Liga Team of the Season: 2016–17, 2019–20
  18. IFFHS World Team of the Decade 2011–2020
  19. IFFHS UEFA Team of the Decade 2011–2020
  20. German Footballer of the Year: 2018
  21. GQ German Athlete of the Year: 2019

Toni Kroos anastaafu akiwa mmoja miongoni mwa viungo bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka. Uwezo wake wa kucheza mpira, akili, na mafanikio yake ya kipekee yanamfanya kuwa gwiji wa kweli. Soka litamkumbuka kama mchezaji aliyebadilisha mchezo na kuweka viwango vipya vya ubora.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Timu zilizowahi Kumaliza Msimu Bila Kufungwa
  2. Yanga SC Kusherehekea Ubingwa wa Ligi kwa Parade Kubwa Mei 25
  3. Tuzo za Ligi Kuu England 2023/24: Hawa Apa washindi wa Tuzo EPL
  4. Liverpool Yamtambulisha Arne Slot Kama Kocha Mpya Rasmi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo