Ratiba Ya Simba Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup 2024/2025

Ratiba Ya Simba Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup 2024/2025: Baada ya kumaliza msimu wa 2023/2024 kwa matokeo mabaya ambayo yameikosesha tiketi ya kufuzu michuano ya CAF Champions League, safari ya Simba SC katika michuano ya CAF Confederation Cup imejulikana rasmi. CAF imetangaza ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) 2024/25, na Simba SC sasa inajiandaa kwa changamoto mpya katika safari yao ya kufikia hatua ya makundi na hatimaye kuwania ubingwa.

Ratiba Ya Simba Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup 2024/2025

Kutokana na wingi wa pointi za CAF walizonazo Simba SC, Wekundu wa Msimbazi wamepata bahati ya kupumzika katika raundi ya awali ya michuano ya CAF Confederation cup ambayo hujulikana pia kama michuano ya kombe la shirikisho CAF.

Hii inamaanisha kuwa Simba Sc wataanzia moja kwa moja kwenye raundi ya pili, ambapo watakutana na mshindi kati ya Uhamiaji FC (Zanzibar) na mshindi wa Kombe la Shirikisho la Libya Libya 1.

Tarehe na Mahali pa Mechi

Simba SC itaanza kampeni yao ya Kombe la shirikisho CAF 2024/2025 kwa kucheza nyumbani na baadaye kusafiri kwa mechi ya marudiano. Hii itatoa fursa kwa mashabiki wa Simba kushuhudia kikosi chao kikifanya kazi ya kupigania nafasi ya kutinga hatua ya makundi.

Washiriki Wengine wa Tanzania

Mbali na Simba SC, Coastal Union pia wanawakilisha Tanzania katika michuano ya CAF Confederation Cup. Coastal Union wataanza kampeni yao kwa kucheza ugenini dhidi ya AS Bravo ya Angola kabla ya kuwaalika nchini kwa mechi ya marudiano. Mshindi wa jumla atakutana na FC Lupopo ya DR Congo kwa mechi nyingine ya nyumbani na ugenini kabla ya kufuzu kwa hatua ya makundi.

Ratiba Kamili Ya Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup 2024/2025

CAF imetangaza rasmi ratiba ya raundi ya pili ya mchujo ya Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025. Michuano hii inatarajiwa kuwa ya yenye ushindani mkubwa huku timu 32 zikichuana vikali ili kujikatia tiketi ya kuingia hatua ya makundi.

Tarehe: Mechi za raundi hii zimepangwa kuchezwa tarehe 13-15 Septemba 2024 (mguu wa kwanza) na 20-22 Septemba 2024 (mguu wa pili).

Ratiba Kamili Kombe la Shirikisho CAF (CAF confederation Cup 2024/2025)

  • M41 & 42: EL KANEMI W. FC 🇳🇬 vs DADJE FC 🇹🇬 vs RS BERKANE 🇲🇦
  • M43 & 44: ASCK 🇹🇬 vs AS FAN 🇳🇪 vs ASEC MIMOSAS 🇨🇮
  • M45 & 46: PAYNESVILLE FC 🇱🇷 vs FOVU DE BAHAM 🇨🇲 vs STADE MALIEN 🇲🇱
  • M47 & 48: HAFIA FC 🇬🇳 vs RAHIMO FC/EFO 🇧🇫 vs ENYIMBA FC 🇳🇬
  • M49 & 50: UTS 🇲🇬 vs RC ABIDJAN 🇨🇮 vs EAST END LIONS FC 🇸🇱 vs ASC JARAAF 🇸🇳
  • M51 & 52: KENYA POLICE FC 🇰🇪 vs ETHIOPIAN COFFEE 🇪🇹 vs ZAMALEK SC 🇪🇬
  • M53 & 54: JAMUS FC/JUBA 🇸🇸 vs STADE TUNISIEN 🇹🇳 vs USMA 🇩🇿
  • M55 & 56: UHAMIAJI FC 🇹🇿 vs LIBYA 1 🇱🇾 vs SIMBA SC 🇹🇿
  • M57 & 58: KITARA FC 🇺🇬 vs LIBYA 2 🇱🇾 vs EL MASRY 🇪🇬
  • M59 & 60: HORSEED FC 🇸🇴 vs RUKINZO FC 🇧🇮 vs CS SFAXIEN 🇹🇳
  • M61 & 62: N. HOTSPURS FC 🇿🇦 vs STELLENBOSCH FC 🇿🇦 vs AS VITA CLUB 🇨🇩
  • M63 & 64: ELGECO PLUS 🇲🇬 vs CD LUNDA-SUL 🇦🇴 vs SEKHUKHUNE UTD 🇿🇦
  • M65 & 66: FC BRAVOS 🇦🇴 vs COASTAL UNION SC 🇹🇿 vs FC LUPOPO 🇨🇩
  • M67 & 68: ALIZE FORT 🇩🇯 vs A. BLACK BULLS 🇸🇿 vs FC 15 DE AGOSTO 🇦🇴 vs AS OTOHO 🇨🇬
  • M69 & 70: FORESTERS FC 🇸🇱 vs ORAPA UNITED 🇧🇼 vs DYNAMOS FC 🇿🇼 vs ZESCO UNITED 🇿🇲
  • M71 & 72: NSOATREMAN FC 🇬🇭 vs TP ELECT SPORT 🇹🇩 vs CS CONSTANTINE 🇩🇿 vs POLICE FC 🇷🇼

Ratiba Ya Simba Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup 2024/2025

Ratiba ya Simba Sc Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho 2024/2025

  • 28/11/2024: Simba vs Bravos.
  • 08/12/2024: Costantine vs Simba.
  • 15/12/2024: Simba vs Sfaxien.
  • 05/01/2025: Sfaxien vs Simba.
  • 12/01/2025: Bravos vs Simba.
  • 19/01/2025: Simba vs Costantine

Tazama hapa Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025 (Caf Confederation Cup Groups)

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2024/2025 Hatua ya Awali
  2. Matokeo Mechi za CECAFA Dar Port Kagame Cup 2024
  3. Makundi ya Dar Port Kagame CECAFA Cup 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo