TAIFA STARS YAWAPA WATANZANIA SABABU YA KUTABASAMU: USHINDI MWEMBAMBA DHIDI YA ZAMBIA WAWAINUA KATIKA SAFARI YA KOMBE LA DUNIA 2026
Taifa Stars Yashinda 1-0 Dhidi ya Zambia
Dar es Salaam, Tanzania – Katika mtanange uliokuwa ukingojewa kwa hamu, Taifa Stars imeonyesha kiwango cha hali ya juu na kuichapa Zambia bao 1-0 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026. Ushindi huu mwembamba lakini muhimu umewapa Watanzania matumaini makubwa ya kutinga fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Kanada, na Mexico.
Waziri Junior, Shujaa wa Siku
Mchezo ulianza kwa kasi huku Taifa Stars wakionyesha dhamira ya kupata ushindi mapema. Dakika ya 4 tu, Waziri Junior Shemtembe aliiandikia Tanzania bao la kuongoza baada ya kumalizia kwa ustadi pasi safi kutoka kwa Mudathir Yahya. Goli hili la mapema liliwapa Taifa Stars nguvu na kuwatia mashabiki kwenye shangwe.
Zambia nao hawakuwa nyuma, walishambulia kwa nguvu wakijaribu kusawazisha. Hata hivyo, safu ya ulinzi ya Tanzania iliyoongozwa na mabeki shupavu akiwemo Ibrahim Bacca chini ya usaidizi wa Bakari Nondo Mwamnyeto iliweza kuhimili mashambulizi yote ya Zambia na kuhakikisha lango lao linabaki salama. Kipa wa Tanzania Ally Salim naye alifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo michache hatari.
Kwa ushindi huu, Taifa Stars sasa inashikanafasi ya pili katika kundi lake la kufuzu ikiwa na pointi 6 nyuma ya Morocco, wakati Zambia inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 3. Hii ni hatua kubwa kwa Tanzania katika safari yao ya kufuzu Kombe la Dunia, na inawapa motisha wa kuendelea kupambana katika michezo ijayo.
Taifa Stars sasa inajipanga kwa mchezo wao ujao wa kufuzu, ambapo watakutana na mpinzani mwingine mkali. Watanzania wana matumaini makubwa kwamba timu yao itaendeleza kiwango hiki kizuri na hatimaye kufikia ndoto ya kushiriki Kombe la Dunia.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Singida Black Stars Yamteua Hussein Masanza Kama Afisa Habari Mpya
- Ratiba ya Kagame CECAFA Cup 2024
- Klabu za Tanzania Zinazoshiriki Kagame Cecafa CUp 2024
- Timu zitakazo shiriki CECAFA kagame Cup 2024
- Tuzo Za Wanamichezo Bora 2024 BMTAwards
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Tetesi za Usajili Real Madrid 2024/2025
- Mshahara wa Kylian Mbappe Real Madrid 2024
- Yanga Yafanikiwa Kutetea Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB 2024
Weka Komenti