Mshahara wa Kylian Mbappe Real Madrid 2024: Mabingwa wa Soka Ulaya Real Madrid wameandika historia nyengine baada ya kutimiza ndoto ya muda mrefu ya mashabiki wao kwa kumsajili mshambuliaji matata Kylian Mbappe. Usajili huu umekua gumzo kubwa katika ulimwengu wa soka, huku Mbappe akitambulika kama mmoja wa wachezaji mahiri na wenye kipaji cha hali ya juu duniani.
Baada ya miaka kadhaa ya uvumi na tetesi, Mbappe ameamua kuondoka Paris Saint-Germain (PSG), klabu aliyoichezea kwa mafanikio makubwa, baada ya mkataba wake kumalizika. Uamuzi huu ulifungua milango kwa klabu nyingi kubwa barani Ulaya kutaka kumsajili, lakini Real Madrid walikuwa wakiongoza mbio hizo kwa muda mrefu.
Los Blancos, kama wanavyojulikana kwa jina la utani, walikuwa wakimmezea mate Mbappe kwa miaka mingi, wakivutiwa na kasi yake ya ajabu, ufundi wa hali ya juu, na uwezo wake wa kufunga mabao ya kila aina. Usajili huu ulmekua ushindi mkubwa kwa Real Madrid, ambao walikuwa wakitafuta mrithi wa Cristiano Ronaldo, ambaye aliondoka klabu hiyo mwaka 2018.
Mshahara wa Kylian Mbappe Real Madrid 2024
Mkataba wa Mbappe na Real Madrid ni wa miaka mitano na unatajwa kuwa na thamani ya €15 milioni (takriban TZS bilioni 39) kwa mwaka baada ya kodi. Hii inamaanisha kuwa Mbappe atakuwa akipokea mshahara wa takriban €288,000 (takriban TZS milioni 750) kwa wiki baada ya makato yote yote ya kodi. Pamoja na kitita cha mshahara wake wa kuvutia, Mbappe pia alipokea ada kubwa ya usajili kutoka kwa Real Madrid. Ingawa kiasi halisi hakijathibitishwa, taarifa zinasema kuwa ada hiyo ilikuwa karibu €150 milioni (takriban TZS bilioni 390).
Mshahara wa Kylian Mbappe Real Madrid Kulinganisha na Mshahara wa PSG
Mshahara wa Mbappe Real Madrid ni mdogo ukilinganishwa na kile alichokuwa akipokea PSG. Huko Paris, mshahara wake wa msingi ulikuwa €75 milioni (takriban TZS bilioni 195) kwa mwaka kabla ya kodi, bila kujumuisha marupurupu mengine. Pia, alipokea bonasi ya usajili ya €100 milioni (takriban TZS bilioni 260) aliposaini mkataba mpya na PSG mwaka 2022.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga Yafanikiwa Kutetea Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB 2024
- Wachezaji wenye Makombe Mengi Ya UEFA
- Idadi ya Makombe ya UEFA Real Madrid
- Viingilio vya Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB 2024: Bei na Maeneo ya Kununua Tiketi Yatangazwa!
- Ley Matampi Golikipa mwenye Clean Sheet Nyingi Ligi Kuu NBC 2023/2024
- Timu za Tanzania Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Timu Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
Weka Komenti