Wachezaji walioachwa na Simba 2024/2025 | Wachezaji wWaliopewa Thank you Simba Sc
Dirisha Kubwa la Usajili la Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 limefunguliwa rasmi, huku Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likisisitiza tarehe ya mwisho ya Agosti 31. Klabu zote zinahitaji kukamilisha usajili wao ndani ya muda huu, ikiwa ni pamoja na uhamisho wa kimataifa kwa wachezaji kutoka nje ya nchi.
Katika kipindi hiki cha usajili, Simba Sports Club, moja ya timu kongwe na maarufu nchini Tanzania, imefanya maamuzi magumu kuhusu wachezaji watakaoachwa kabla ya msimu mpya kuanza. Hii ni baada yakutokua na msimu mzuri baada ya kumaliza ligi katika nadfasi ya tatu na kushindwa kubeba makombe yaliokua katika mipango yao.
Simba, iliyoanzishwa mwaka 1936 na kubeba mataji 22 ya Ligi Kuu, mara 6 ya Kombe la Kagame, na mara 18 ya ubingwa wa taifa, inajulikana kwa ushindani wake mkali, haswa dhidi ya watani wao wa jadi, Young Africans.
Ni jambo la kawaida kwa klabu kubwa kama Simba kufanya mabadiliko katika kikosi chao kila msimu, ili kuimarisha timu na kushindana vyema katika mashindano mbalimbali. Hata hivyo, maamuzi ya kuachana na wachezaji fulani huwa magumu na mara nyingi huzua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki.
Katika makala haya, Habariforum.com inakuletea orodha kamili ya wachezaji walioachwa na Simba SC kuelekea msimu mpya wa 2024/2025, pamoja na uchambuzi wa kina kuhusu athari za mabadiliko haya kwenye kikosi cha timu hiyo.
Hawa Ndio Wachezaji walioachwa na Simba 2024/2025
1. John Bocco
Simba SC imeamua kuachana na nahodha wao mkongwe, John Bocco, kufuatia kushuka kwa kiwango chake cha uchezaji. Licha ya kuwa kocha wa timu ya vijana ya Simba, Bocco ameitumikia klabu hiyo kwa miaka saba na amekuwa mchezaji wa kwanza kupewa “Thank You na Simba” katika kipindi hiki cha usajili.
Kuondoka kwa Bocco kutaacha pengo kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba, kwani alikuwa mmoja wa wafungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo lakini bado kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana na mrithi wake katika dirisha hili la usajili.
2. Saido Ntibazonkiza
Kiungo mshambuliaji raia wa Burundi, Saido Ntibazonkiza, amemaliza mkataba wake na Simba SC na hataendelea kuichezea klabu hiyo msimu ujao. Ntibazonkiza alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha Simba, akiisaidia timu hiyo kutwaa mataji mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili aliyoitumikia.
3. Shaban Idd Chilunda
Mshambuliaji Shaban Idd Chilunda amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na Simba SC na hatakuwa sehemu ya kikosi cha msimu ujao. Chilunda alijiunga na Simba mwaka 2023 akitokea Azam FC, lakini hakupata nafasi ya kutosha ya kucheza kutokana na ushindani mkali katika safu ya ushambuliaji. Kuondoka kwake kutaipa Simba nafasi ya kusajili mshambuliaji mpya atakayeweza kuimarisha safu hiyo.
Luis Miquissone
Klabu ya Simba SC imeachana na aliyekuwa Kiungo Mshambuliaji wake,Luis Miquissone kufuatia kiwango kibovu alichoonyesha nyota huyo tangu amesajiliwa na Simba kwa mara ya pili. Miquissone alijiunga na Simba dirisha kubwa la msimu uliopita akitokea katika Klabu ya Al Ahly ya Misri ambako alishindwa kuwashawishi na hivyo kuvunja nae Mkataba.)
Kennedy Juma
Baada ya miaka mitano aliyodumu ndani ya klabu ya Simba, mlinzi wa kati Kennedy Wilson Juma hatokuwa sehemu ya kikosi cha Mnyama kuelekea msimu mpya baada ya mkataba wake kumalizika. Kennedy Juma alijiunga na Simba Julai 2019 akitokea katika Klabu ya Singida United ya Mkoani Singida. Kwa sasa Kennedy Juma anatajwa kumalizana na Klabu ya Coastal Unioni ambao
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti