Huu Apa Wimbo Mpya wa Nay Wa Mitego Ft Raydiace – Nitasema
Muimbaji mahiri wa muziki wa Hip Hop kutoka Tanzania, Nay Wa Mitego, ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Nitasema akiwa amemshirikisha msanii mwingine wa Bongo Fleva, Raydiace. Huu ni miongoni mwa vibao ambavyo vimeonesha kugusa nyoyo za wengi, hasa kutokana na ujumbe wake mzito unaozungumzia matukio mbalimbali yanayoendelea nchini, mabadiliko na haki katika jamii.
Katika wimbo huu, Nay Wa Mitego anajichukulia jukumu la kuisemea jamii ambayo imeshindwa kupaza sauti kukemea mambo mbalimbali yanayojitokeza, hata kama ukweli huo unaweza kusababisha matatizo au kutokubalika kwa baadhi ya watu.
Raydiace, ambaye ni mwimbaji anayekuja juu kwa kasi katika tasnia ya Bongo Fleva, ameongeza ladha ya kipekee kwenye wimbo huu, huku sauti yake ya kipekee ikifanya wimbo kuwa mzuri zaidi na kupendwa na mashabiki wengi wa muziki wa kiharakati.
Nay Wa Mitego Ft Raydiace – Nitasema
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti