Wasanii Wa Afrika Walioshinda Tuzo Za BET 2024 | Tumekuletea orodha ya Waafrika walioshinda tuzo za BET 2024
Bara la Afrka limeheshimishwa kwa mara nyingine tena katika usiku wa kihistoria wa Tuzo za BET ambazo ulifanyika Usiku wa Juni 30, kwenye ukumbi wa Peacock Theater mjini Los Angeles, California. Mashabiki wa muziki mzuri kutoka bara la Afrika walipata sababu ya kujivunia tena baada ya kushuhudia wasanii wao pendwa wakiibuka washindi wa tuzo mbalimbali.
Tuzo za BET ni miongoni mwa tuzo za muziki zenye umaarufu na heshima kubwa katika tasnia na muziki Duniani. Tuzo hizi, zilianzishwa mwaka wa 2001 na televisheni ya Black Entertainment Television (BET), na kua jukwaa la kipekee kwa ajili ya kusherehekea vipaji vya watu weusi katika nyanja mbalimbali, ikiwemo muziki, filamu, michezo, na uhisani.
Waamuzi wa tuzo za mwaka huu, ambao walikuwa wataalamu kutoka kwenye tasnia za muziki, vyombo vya habari, michezo, na sanaa kwa ujumla, walichagua orodha ya wasanii walioteuliwa kuwania vipengele mbalimbali kutokana na ubora na vipaji walivyo onesha. Hapa tumekuletea orodha ya wasanii wa Afrika walioshinda Tuzo za BET 2024.
Wasanii Wa Afrika Walioshinda Tuzo Za BET 2024
Katika usiku wa Tuzo za BET 2024, Afrika Kusini ndio nchi ya Afrika ambayo iliyo ibua washindi walioiwakilisha AFrika, kipenzi kipya cha wapenzi wa muziki Duniani Tyla akishinda tuzo mbili kubwa – Msanii Bora Chipukizi na Msanii Bora wa Kimataifa. Wimbo wake maarufu “Water,” uliotikisa dunia nzima, ulichangia pakubwa katika ushindi wake.
Aidha, msanii mwenzake kutoka Afrika Kusini, Makhadzi, alijishindia tuzo ya Chaguo la Watazamaji: Msanii Mpya Bora wa Kimataifa.
Nigeria imeendelea kutamba katika ukumbi wa BET baada ya Tems kuiwakilisha vyema ambapo aliibuka kidedea kwa wimbo wake “Me & U,” akishinda tuzo ya Dr Bobby Jones Best Gospel/Inspirational Award.
Tuzo Walizoshinda Wasanii wa Afrika BET 2024
Usiku wa tuzo za BET 2024 ulikuwa wa kihistoria kwa wapenzi na wafuatiliaji wa muziki wa Afrika, huku wasanii kadhaa kutoka Afrika wakishinda tuzo kubwa. Hapa tumekuletea orodha kamili ya washindi wa tuzo za BET 2024 kutoka Afrika.
1. Tuzo ya Msanii Mpya Bora (Best New Artist)
Katika Tuzo za BET 2024, wasanii wapya walionyesha uwezo mkubwa na ubunifu wao, na kuifanya kipengele hiki kuwa na ushindani mkali. Mshindi wa tuzo ya Msanii Mpya Bora ni Tyla, aliyewapiku wenzake kwa ubora wa kazi zake. Orodha kamili ya walioteuliwa ni:
- 4Batz
- Ayra Starr
- Bossman DLow
- Fridayy
- October London
- Sexyy Red
- Tyla – MSHINDI
2. Tuzo ya Msanii Bora wa Kimataifa (Best International Act)
Kipengele hiki kilikuwa na wasanii mahiri kutoka pembe zote za dunia. Ushindi wa Tyla unathibitisha umahiri wake katika muziki wa kimataifa. Walioteuliwa ni:
- Asake (Africa)
- Aya Nakamura (France)
- Ayra Starr (France)
- BK (Brazil)
- Cleo Sol (UK)
- Focalistic (Africa)
- Karol Conka (Brazil)
- Raye (UK)
- Tiakola (France)
- Tyla (Africa) – MSHINDI
3. Tuzo ya Chaguo la Watazamaji Msanii Bora wa Kimataifa (Viewers’ Choice Best International Act)
Makhadzi kutoka Afrika kusini alichaguliwa kama Msanii Bora wa Kimataifa na watazamaji, akionesha jinsi alivyopendwa na mashabiki. Walioteuliwa ni:
- Bellah (UK)
- Cristale (UK)
- Duquesa (Brazil)
- Holly G (France)
- Jungeli (France)
- Makhadzi (Africa) – MSHINDI
- Oruam (Brazil)
- Seyi Vibez (Africa)
- Tyler Icu (Africa)
4. Dr. Bobby Jones Best Gospel/Inspirational Award
Katika kipengele cha muziki wa Injili na nyimbo zenye ujumbe wa kiroho, Tems aliibuka mshindi kwa wimbo wake “Me & U.” Hawa ndio walioteuliwa:
- Shirley Caesar – All Of The Glory
- Kirk Franklin – All Things
- Halle Bailey – Angel
- Cece Winans – Come Jesus Come
- Erica Campbell – Do You Believe In Love?
- Maverick City Music, Naomi Raine, & Chandler Moore – God Problems
- Tems – Me & U – MSHINDI
- Kirk Franklin – Try Love
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti