Washindi wa Tuzo Za ZFF PBZ AWARDS 2024 | Tuzo Za Ligi Kuu Zanzibar 20233/2024
Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) limetangaza washindi wa tuzo za kifahari za ZFF PBZ Awards 2024, zikitambua na kusherehekea wachezaji, makocha, na waamuzi walioonyesha kiwango cha hali ya juu cha ubora na kujituma katika msimu wa 2023/2024 wa ligi kuu ya soka Zanzibar. Tuzo hizi zimekua zikitolewa kila baada ya msimu kumalizika likiwa na lengo kuu la kutoa motisha kwa wadau wa soka Zanzibar kufanya vizuri ili kuweza kupata heshima ya kutangazwa bingwa wa tuzo hizo.
Hafla ya kukabidhi tuzo za ZFF PBZ awards kwa mwaka huu 2024 ilifanyika Jumamosi, tarehe 29 Juni 2024, katika ukumbi wa kifahari wa Hotel Verde visiwani Zanzibar. Sherehe hizo zilikuwa kilele cha msimu uliokuwa na ushindani mkali, zikiwapa heshima wale waliojitokeza na kuacha alama isiyofutika katika vitabu vya kihishoria ya soka la Zanzibar.
Hapa tumekuletea orodha ya washindi wote wa Tuzo za ZFF PBZ awards 2024.
Washindi wa Tuzo Za ZFF PBZ AWARDS 2024
Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar Ni Suleiman Mwalim Abdallah
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar msimu wa 2023/24 ametangazwa kuwa Suleiman Mwalim Abdallah, nyota anayeng’ara wa KVZ. Mwalim amekuwa kiungo muhimu katika mafanikio ya timu yake msimu huu, akionyesha uwezo wa hali ya juu wa uchezaji, ubunifu, na kuamua matokeo ya mechi kwa uwezo wake mkubwa wa kuziona nyavu za wapinzani.
Sio tu kwamba Mwalim ameibuka mchezaji bora wa ligi kuu ya Zanzibar (PBZ premier league) 2023/2024, bali pia amemaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo kwa kufunga mabao 20, akithibitisha kuwa ni mshambuliaji hatari na mwenye uwezo mkubwa wa kufumania nyavu. Tuzo hii ni ushahidi tosha wa mchango wake mkubwa katika soka la Zanzibar.
Kikosi bora cha msimu ligi kuu ya Zanzibar 2023/2024
Alex Gideon, Shaban Pandu Hassan, Swed Juma Hussein, Abdulrahim Seif Bausi, Isihaka Rashid Mwinyi, Abdallah Yassin Kulandana, Abdulmafudh Mohamed Ally, Hussein Mwinyi Deco, Ibrahim Isihaka, Ibrahim Ahmada Hilika, Suleiman Mwalimu Abdallah
Tuzo Ya Kiungo Bora wa Ligi Kuu Zanzibar 2023/2024
Mshindi wa Tuzo Ya Kiungo Bora wa Ligi Kuu Zanzibar 2023/2024 ni Abdalla Yassin Kulandana wa Mlandege
Tuzo Ya Muandishi Bora wa ZFF PBZ Award 2023/2024
Mwandishi mahiri wa Gazeti la Zanzibar Leo, Mwajuma Juma, ameibuka mshindi wa tuzo ya Muandishi Bora wa Ligi Kuu Zanzibar 2023/2024 katika usiku wa ZFF PBZ Awards 2023-24. Tuzo hii imetolewa kwa lengo la kutambua mchango wake mkubwa katika kuripoti habari za soka kwa weledi, umakini, na ubunifu, akileta habari za ligi kuu karibu na mashabiki wa soka visiwani Zanzibar.
Mshindi wa Tuzo Ya Msemaji Bora wa Timu ni Idrissa Yakuti wa New City
ZFF PBZ AWARDS | Goli bora la Msimu La PBZ Premier League 2023/24.
Goli bora la msimu wa 2023/2024 wa ligi kuu ya Zanzibar limetolewa kwa Ali Khatib Inzaghi, mshambuliaji mahiri wa Uhamiaji FC. Bao hilo la kusisimua lilipachikwa wavuni katika mchezo mkali dhidi ya JKU, likionyesha ustadi wa hali ya juu na ubunifu wa Inzaghi uwanjani.
ZFF PBZ AWARDS | Goli bora la msimu kwenye #PBZPremierLeague 2023/24.
Goli limetoka kwa Ali Khatib Inzaghi wa Uhamiaji FC alilofunga kwenye mchezo dhidi ya JKU.
Tuzo nyingine zinazotoka hapa ni Beki Bora na Kiungo Bora. .
Ni katika Usiku wa Tuzo za ZFF na PBZ uliofanyika… pic.twitter.com/spnUw9G2Rx
— Azam TV (@azamtvtz) July 1, 2024
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti