Matokeo ya Yanga Vs KMC Leo 29 September 2024 | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya KMC FC
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC Tanzania, Wananchi leo wanashuka wataikalibisha KMC Fc uwanja wake wa nyumbani, Azam Complex, Chamazi katika mchezo wa ligi ambao wao wenyewe wanasema ni JUMAPILI YA KUFOSI.
Yanga wataikabili KMC wakiwa na kumbukumbu ‘mujarabu’ ya kushinda kwa jumla ya magoli manane kwenye michezo miwili ya NBC Premier League msimu uliopita. Walianza Agosti 23, 2023 ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa magoli 5-0 kwenye mchezo ambao wao walikuwa wenyeji. Februari 17, 2024 wakakutana tena wawili hawa na matokeo yakawa 0-3, Yanga ikiwa ugenini.
Yanga SC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya KMC. Katika mechi 12 zilizopita za Ligi Kuu walizokutana, Yanga imeshinda mara 9, KMC ikibeba ushindi mara moja tu, huku mechi mbili zikiishia kwa sare. Hii inaonyesha ni jinsi gani Yanga imekuwa na ubabe dhidi ya KMC, na historia hii inaweza kuipa Yanga motisha zaidi ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo.
Yanga imeanza msimu wa 2024/2025 kwa kishindo, ikiibuka na ushindi kwenye mechi zake zote mbili za awali za Ligi Kuu, ikifunga mabao matatu na bila kuruhusu bao lolote kufungwa. Pia Yanga Sc imefungwa bao moja tu katika mechi nane za mashindano mbalimbali tangu msimu uanze wakati safu yake ya ushambuliaji, ikifunga mabao 25 kwenye mechi hizo, jambo linalowafanya kuwa tishio kwa timu pinzani.
Matokeo ya Yanga Vs KMC Leo 29 September 2024
Yanga | 1-0 FT | KMC Fc |
|
- 🏆 #NBCPremierLeague
- ⚽️ Young Africans SC🆚KMC FC
- 📆 29.09.2024
- 🏟 Azam Complex
- 🕖 21:00 (EAT)
Katika mechi ya mwisho ya ligi, Yanga iliwalaza KenGold kwa bao 1-0, baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 2-0 ugenini. Mfululizo huu wa ushindi unaifanya Yanga kuingia kwenye mchezo huu dhidi ya KMC wakiwa na hali ya kujiamini. Kwa upande wa KMC, hali si shwari sana. Timu hii haijaonyesha uwezo wa kuvutia tangu msimu uanze, ikiwa imeshinda mechi moja tu, kutoka sare moja, na kupoteza mechi tatu. KMC imefunga mabao matatu tu huku ikiruhusu mabao saba kufungwa, jambo linaloashiria udhaifu katika safu yao ya ulinzi.
Hata hivyo, mchezaji wa kutegemewa kwa KMC, Redemptus Musa, amekuwa nguzo muhimu katika kikosi hicho, akifunga mabao mawili kati ya matatu ya timu yake msimu huu. Musa anatarajiwa kuwa mchezaji wa kuangaliwa zaidi kwenye mchezo huu, huku akihitajika kuonyesha makali yake dhidi ya safu ya ulinzi ya Yanga ambayo haijaruhusu mabao mengi msimu huu.
Historia ya mechi za Yanga Dhidi ya KMC
- Michezo 12
- Ushindi 9
- Sare 2
- Kupoteza 1
- Magoli Kufunga 21
- Magoli Kufungwa 5
- Cleansheet 7
Umuhimu wa Mchezo kwa Yanga na KMC
Kwa Yanga, ushindi kwenye mchezo huu utawapa nafasi nzuri ya kuendelea kuongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuimarisha nafasi yao ya kutetea ubingwa. Kwa KMC, ni nafasi ya kujitahidi kurekebisha hali yao ya msimu huu na kupata alama muhimu kwenye ligi, ingawa watakutana na changamoto kubwa kutoka kwa mabingwa watetezi.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti