Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
Mashindano ya Kombe la Muungano 2026 yanaendelea kushika kasi visiwani Zanzibar, huku hatua ya robo fainali ikiwa inaelekea tamati huku mechi mbili pekee zikiwa zimesalia kufikia leo april 22 2026. Hata hivyo, tayari baadhi ya timu zimeonyesha ubora wao mapema kwa kufuzu hatua ya nusu fainali, jambo linaloongeza ushindani mkubwa kuelekea hatua za mwisho za michuano hiyo.
Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026 (Mpaka Sasa)
Kwa mujibu wa matokeo yaliyopatikana hadi sasa, timu mbili tayari zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali:
- Azam FC
- Yanga SC (Mabingwa watetezi)
Azam FC Yafuzu Baada ya Kuifunga KVZ
Azam FC ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Uwanja wa New Amaan. Mabao yote yalifungwa na mshambuliaji Jean Ngita, aliyefunga bao la kwanza dakika ya 40 na kuongeza la pili dakika ya 54.
Matokeo hayo yameihakikishia Azam FC nafasi ya kucheza nusu fainali, ikiwa ni moja ya timu zilizoonyesha kiwango bora katika hatua hii ya mashindano.
Yanga SC Yaendelea Kuonyesha Ubora
Kwa upande mwingine, Yanga SC ilitinga nusu fainali baada ya ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Muembe Makumbi City. Mabao hayo yalifungwa na Prince Dube (mawili), pamoja na Kwabena Frank Assinki na Shekhan Ibrahim Khamis.
Ushindi huo unaendelea kuthibitisha uimara wa Yanga SC kama mabingwa watetezi wa Kombe la Muungano.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply