Kikosi cha Yanga Vs Azam Leo 25/04/2026
Wana rambaramba Azam FC leo watakuwa wenyeji wa Yanga SC katika pambano la nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Muungano litakalopigwa katika dimba la Amaan Complex, Zanzibar. Mchezo huu wenye hadhi ya juu unatarajiwa kuanza saa 2:15 usiku, ukiwa na mvuto mkubwa kutokana na ubora wa timu hizi mbili zinazowania nafasi ya kutinga fainali.
Muhtasari wa Mchezo
Huu ni mchezo unaobeba uzito wa kipekee, ambapo Yanga SC inaingia kama bingwa mtetezi wa mashindano haya baada ya kutwaa taji msimu uliopita kwa kuifunga JKU bao 1-0. Kwa upande mwingine, Azam FC inaingia ikiwa na lengo la kuandika historia mpya kwa kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Kombe la Muungano. Katika hatua ya robo fainali, Yanga ilionyesha ubora wake baada ya kuifunga Muembe Makumbi City mabao 4-0, huku Azam FC ikifuzu baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya KVZ.
Kikosi cha Yanga Vs Azam Leo 25/04/2026
Kikosi cha wananchi kinachoanza katika mchezo huu wa nusu fainali kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa moja usiku huku mashabiki wengi wakitarajia kuona kikosi chenye nguvu ambacho kitaingia uwanjani kwa malengo ya kuhakikisha ushindi katika dakika za awali za mchezo huu muhimu wa Kombe la Muungano. Hadi sasa, hakuna orodha rasmi ya wachezaji iliyotolewa kabla ya mchezo, jambo linalomaanisha kuwa maamuzi ya mwisho yatatolewa na benchi la ufundi muda mfupi kabla ya mchezo kuanza.
Hii ni kawaida katika michezo ya hatua ya juu kama nusu fainali, ambapo makocha hutumia mbinu za mwisho kulingana na maandalizi na hali ya wachezaji. Mashabiki wa Yanga SC wanatarajia kuona kikosi chenye uwiano mzuri kati ya uzoefu na nguvu ya vijana, ambacho kitaweza kushindana katika mchezo huu mgumu dhidi ya Azam FC. Kwa upande wa Azam FC pia, mabadiliko ya kikosi yanaweza kuonekana kulingana na mbinu za mchezo na hali ya wachezaji wake muhimu.
Kwa ujumla, kikosi kitakachotangazwa kitakuwa na jukumu kubwa la kuamua mwelekeo wa mchezo huu wa nusu fainali, ambao una uzito mkubwa katika safari ya kuelekea fainali ya Kombe la Muungano.
Hiki Apa Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Azam Fc
- 39. Diarra
- 33. Mwenda
- 23. Boka
- 36. Assinki
- 4. Bacca (C)
- 25. Damaro
- 7. Maxi
- 38. Abuya
- 29. Dube
- 20. Okello
- 10. Pacome
Wachezaji wa Akiba: Masalanga, Yao, Andabwile, Sheikhan, Faridi, Edmund, Mudathir, Kouma, Depu
Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo
Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema kuwa wanakutana na timu ngumu na yenye takwimu bora kwenye ligi. Ameeleza kuwa Azam imejiandaa kucheza mchezo mgumu na kutumia mbinu zao za kawaida ili kupata matokeo.
Kwa upande wa Yanga SC, kocha Pedro Goncalves amesema Azam ni timu yenye nguvu, uwekezaji mkubwa na wachezaji wazuri, hivyo wanatarajia mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa. Ameongeza kuwa lengo lao ni kushinda na kuendelea hatua ya fainali.
Rekodi na Mwenendo wa Timu
Katika ligi kuu, timu zote mbili hazijapoteza mchezo wowote, jambo linaloonyesha uimara wao. Matokeo yao mabaya yamekuwa ni sare pekee.
Katika historia ya mikutano yao nje ya ligi, wamekutana mara 17 ambapo:
- Yanga imeshinda mechi 10
- Azam imeshinda mechi 5
- Sare zikiwa 2
Msimu huu pekee, tayari wamekutana mara mbili:
- Yanga ilishinda fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa penalti 5-4
- Mchezo wa ligi uliisha kwa sare tasa
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
- Matokeo ya Simba vs Mafunzo leo 23/04/2026
- Ratiba ya Kombe la Muungano Leo 23/04/2026
- Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
- Vilabu Bora Afrika 2026/2027 (CAF Club Ranking)
- CAF Rankings 2026: Simba Yaporomoka, Yanga Yaendelea Kung’ara Afrika








Leave a Reply