Kikosi cha Simba Vs Mlandege Leo 26/04/2026
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi leo kitashuka dimbani kuisaka tiketi ya fainali ya Kombe la Muungano, ambapo kitakutana uso kwa uso na mabingwa wa Zanzibar, Mlandege FC, katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mchezo huo wa nusu fainali ya pili unapigwa leo, Aprili 26, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 2:15 usiku.
Simba inakwenda katika mchezo huo ikiwa na lengo la kufanya vizuri na kufuta matokeo yaliyowahi kuiumiza dhidi ya Mlandege katika mechi zao za nyuma. Kwa upande mwingine, Mlandege nayo imejipanga kulinda heshima ya Zanzibar na kuendeleza rekodi yake nzuri mbele ya mabingwa hao wa Dar es Salaam.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara waliingia hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa Aprili 23, 2026. Bao pekee la ushindi wa Simba lilifungwa na mshambuliaji Seleman Mwalimu ‘Gomes’ dakika ya 53, baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Baraka Mwangosi.
Ushindi huo uliifanya Simba kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea na safari yake ya Kombe la Muungano, michuano ambayo inatazamwa kama fursa muhimu ya kulitafutia taji la kwanza la msimu huu. Klabu hiyo inatafuta ubingwa wa kwanza msimu huu ikiwa bado ina matumaini kwenye michuano mingine iliyosalia.
Katika mchezo wa robo fainali, Simba ilianza na kikosi chenye wachezaji wengi ambao hupata nafasi ndogo kwenye mechi za Ligi Kuu Bara. Hata hivyo, licha ya kufanya vizuri kwa ujumla, timu hiyo ilikosa makali ya kupata ushindi mkubwa zaidi.
Historia ya Mlandege dhidi ya Simba
Mchezo wa leo una uzito zaidi kutokana na kumbukumbu ya mechi za nyuma kati ya timu hizi mbili. Mlandege ndiyo timu iliyomuumiza Simba mara mbili kwenye matukio ya nyuma, na hilo linaifanya mechi hii kuingia katika hesabu maalum kwa wekundu wa Msimbazi.
Mara ya kwanza kukutana katika Kombe la Mapinduzi 2023, Simba ilitolewa kwa penalti katika hatua ya nusu fainali baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Mlandege kisha ikaenda kuchukua ubingwa baada ya kuifunga Singida kwa mabao 2-1 kwenye fainali.
Msimu uliofuata wa 2024, Mlandege iliifunga tena Simba kwa bao 1-0 katika fainali ya mashindano hayo, bao lililofungwa na Joseph Akondwanao ambaye kwa sasa anaitumikia TRA United. Historia hiyo inatosha kuonyesha kwa nini Simba inaingia leo ikiwa na tahadhari kubwa.
Kikosi cha Simba Vs Mlandege Leo 26/04/2026
Kikosi cha Simba kitakachoanza leo dhidi ya Mlandege FC kinatarajiwa kutangazwa na benchi la ufundi majira ya saa moja punde kabla ya mchezo kuanza. Hatua hiyo ni sehemu ya utaratibu wa mwisho wa maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Muungano unaopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 2:15 usiku.
Simba inaelezwa kuingia uwanjani ikiwa na hesabu maalum za ushindi kutokana na ushindani mkali uliopo kati yake na Mlandege, pamoja na historia ya matokeo ya nyuma ambayo imekuwa changamoto kwa Wekundu wa Msimbazi. Kocha Steven Barker ameweka wazi kuwa timu yake imejipanga kikamilifu kuhakikisha inafikia malengo ya kusonga mbele hadi fainali bila kujali uzito wa mpinzani.
Hiki Apa Kikosi cha Simba Kilichotangazwa Leo Dhidi ya Mlandege
- 28 ABEL
- 15 DUCHU
- 5 MLIGO
- 60 MBEGU
- 23 DE REUCK
- 8 KANTE
- 27 BAJABER
- 35 MAEMA
- 34 MPANZU
- 18 MORICE
- 63 BASHIRI
WACHEZAJI WA AKIBA: KASSALI, KAPOMBE, TOURE, KAGOMA, GUEYE, CHAMA, MWALIMU, INNO, OURA.
Katika mchezo uliopita wa robo fainali, Simba ilitumia kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji waliopata nafasi chache katika ligi, lakini bado ikaonesha uimara na kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mafunzo kupitia Seleman Mwalimu ‘Gomes’. Ushindi huo uliiwezesha timu hiyo kufuzu hatua ya nusu fainali na kukutana na Mlandege.
Kwa upande wa wachezaji, uwepo wa Mohamed Bajaber ambaye alirejea uwanjani baada ya majeraha unatarajiwa kuongeza chaguo la kiufundi katika eneo la kiungo mshambuliaji. Bajaber alicheza dakika 45 za kipindi cha pili katika mchezo wa robo fainali, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana uwanjani tangu Januari 18, 2026.
Matarajio yanaonesha kuwa kikosi cha Simba kitakuwa na mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu na wale wanaopata nafasi ya kujidhihirisha, huku benchi la ufundi likijaribu kupata uwiano sahihi wa ushindani na matokeo chanya.
Kwa ujumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa mtihani mgumu kwa Simba kutokana na ubora wa Mlandege pamoja na rekodi yake ya kuisumbua timu hiyo katika mashindano ya nyuma, hivyo kikosi kitakachotangazwa kitakuwa na jukumu kubwa la kubeba matumaini ya mashabiki kuelekea fainali ya Kombe la Muungano.
Mlandege yapania kulinda heshima ya Zanzibar
Mlandege, ambayo ilikuwa timu pekee ya Zanzibar iliyofika hatua ya nusu fainali katika michuano hiyo, imebeba matumaini ya visiwani baada ya kuzitoa timu za Muembe Makumbi City, KVZ na Mafunzo zilizoishia robo fainali. Hiyo inaiweka timu hiyo katika nafasi ya kulinda hadhi ya Zanzibar kwenye mashindano haya.
Timu hiyo imekuwa na mashabiki wengi kwenye hatua za robo fainali, jambo linaloipa nguvu ya ziada kabla ya kukutana na Simba. Mlandege inatarajiwa kutegemea wachezaji wake wa mkopo kutoka Azam FC ambao wamekuwa wakionesha ubora mkubwa, akiwemo beki Vellim Opondo, Mahmoud Haji, fundi wa pasi Jamal Saleh pamoja na washambuliaji Mussa Hassan na Omar Juma, walioifungia timu hiyo mabao yaliyoipeleka nusu fainali.
Kocha Hassan Ramadhan amesema kikosi chake kiko tayari kwa mechi hiyo na kwamba wamejiandaa katika kila nyanja kuhakikisha wanatinga fainali kwa kuwang’oa wekundu wa Msimbazi.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply