Hizi Ndio Timu 5 Ambazo Bado Hazijashinda Mechi yoyote Ligi Kuu
Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 inaendelea kua chanzo cha furaha na uzuni kwa mashabiki wengi wa soka la Tanzania, huku baadhi ya timu zikijipatia matokeo bora na nyingine zikiendelea kusaka ushindi wao wa kwanza.
Hadi kufikia hatua ya mzunguko wa tano ya ligi, timu tano bado hazijafanikiwa kupata ushindi wowote katika michezo waliokwisha cheza. Timu hizi zimepambana lakini bado hazijapata ladha ya ushindi, jambo ambalo limezua maswali miongoni mwa wadau wa soka nchini.
Timu hizo tano ni Prisons, Pamba Jiji, JKT Tanzania, Coastal Union, na KenGold. Hapa tutazama kwa undani juu ya kila timu na mwenendo wao hadi sasa, na kwa nini bado hazijapata ushindi.
1. Prisons
Timu ya Prisons, ambayo inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi, imecheza michezo minne bila kushinda.
Hata hivyo, timu hii imeonyesha uwezo wa kujilinda kwa kutoa sare katika michezo yote, na kujikusanyia jumla ya pointi nne. Hali hii inaashiria kwamba Prisons inajitahidi kutopoteza michezo, lakini ina changamoto katika kumalizia na kupata ushindi.
2. Pamba Jiji
Pamba Jiji, ambayo imepanda daraja msimu huu, tayari imeshacheza michezo mitano lakini haijafanikiwa kushinda hata mmoja.
Pamba Jiji imetoa sare nne na kupoteza mchezo mmoja, na kwa sasa inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi nne. Pamba Jiji imeonyesha ukomavu wa kupambana, lakini bado inahitaji kuboresha safu ya ushambuliaji ili kufanikisha ushindi wa kwanza.
3. JKT Tanzania
JKT Tanzania nayo ipo katika kipindi kigumu, ikiwa imetoa sare katika michezo yote mitatu iliyocheza hadi sasa.
Timu hii inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tatu. Wataalamu wa soka wanahoji iwapo JKT Tanzania inaweza kuvunja mwiko wa sare na kupata ushindi katika mechi zijazo.
4. Coastal Union
Coastal Union, ambayo inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi, imecheza michezo minne bila kushinda.
Wagosi wa Kaya wametoa sare moja tu na kupoteza michezo mitatu, na kujiukuta miongoni mwa timu zilizo na matokeo yasiyoridhisha hadi sasa. Coastal Union inakabiliwa na changamoto ya kuimarisha ulinzi na ushambuliaji ili kuepuka kushuka daraja msimu huu.
5. KenGold
Timu ya KenGold kwa sasa inashika mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa haina pointi hata moja. KenGold imeshacheza michezo minne, ikipoteza yote bila kufanikiwa kufunga mabao ya kutosha. Hii ni timu inayokabiliwa na changamoto kubwa, na inahitaji kubadilisha mbinu zake ili kurejea kwenye ushindani wa ligi kuu.
Timu Zinazofanya Vyema Ligi Kuu Hadi Sasa
Tukiachana na timu hizi tano ambazo bado hazijashinda, kuna timu ambazo zinajiimarisha vilivyo kwenye msimamo wa ligi. Mfano bora ni Singida Black Stars, ambayo imepata ushindi katika michezo yote minne iliyocheza mpaka sasa.
Ushindi huu umeiweka Singida katika nafasi nzuri ya kushindania taji la Ligi Kuu msimu huu. Pia, timu kama Simba SC na Yanga SC zinaendelea kufanya vizuri, zikiwapa changamoto timu nyingine kwenye mbio za ubingwa.
Mapednekezo ya Mhariri:
Weka Komenti