CV ya Fadlu Davids: Kocha Mpya wa Simba SC (2024/2025)
Klabu ya Simba SC imemtangaza rasmi kocha wao mpya atakae iongoza klabu kwenye msimu wa 2024/2025. Baada ya mazungumzo yaliodumu takribani wiki moja, hatimaye Simba Sc imefanikiwa kunasa saini ya Fadlu Davids na kumtangaza rasmi kama kocha wao mkuu mpya kuelekea msimu wa 2024/2025, akichukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa muda, Juma Mgunda. Uteuzi huu unakuja baada ya kipindi cha mabadiliko ndani ya klabu, ambapo kocha wa awali, Abdelhak Benchikha, aliondoka kutokana na changamoto za kifamilia.
Fadlu Davids, kocha mwenye uzoefu mkubwa kutoka Afrika Kusini, anatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika kikosi cha Simba SC. Akiwa na rekodi ya kuongpoza timu kama Orlando Pirates na Maritzburg United, pamoja na uzoefu wake kama kocha msaidizi katika klabu za kimataifa kama Raja Casablanca na Lokomotiv Moscow, Davids anaingia Msimbazi akiwa na CV ya kuvutia.
Uteuzi huu unaashiria nia ya Simba SC kurejesha makali yao katika soka la ndani na kimataifa CAF. Mashabiki wa Simba wana matumaini makubwa kwamba Fadlu Davids ataleta mbinu mpya na uongozi utakaowezesha klabu kufikia malengo yake makubwa, ikiwemo kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa kama vile Kombe la Shirikisho Afrika na AFL.
Je, Fadlu Davids ataweza kutimiza matarajio haya makubwa? Je, mtindo wake wa ukocha unaendana na falsafa ya Simba SC? Katika makala haya, tutaangazia kwa undani wasifu wa Fadlu Davids (CV ya Fadlu Davids), uzoefu wake wa ukocha, mtindo wake wa uongozi, na matarajio makubwa yanayomzunguka katika klabu ya Simba SC.
CV ya Fadlu Davids: Kocha Mpya wa Simba SC (2024/2025)
Jina Kamili | Fadluraghman Davids |
Tarehe ya Kuzaliwa | Mei 21, 1981 (43) |
Mahali pa Kuzaliwa | Cape Town, Western Cape Afrika Kusini |
Uraia | Afrika Kusini |
Muda wa Kawaida Kama Kocha | Miaka 0.50 |
Leseni ya Ukocha | Leseni ya UEFA Pro |
Mfumo Anaoupenda | 4-2-3-1 |
Uzoefu wa Ukocha wa Fadlu Davids (Timu Alizowahi Kuwa Kocha)
Fadlu Davids ni miongoni mwa makocha wenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika Kusini. Akiwa kama Kocha mkuu na kocha msaidizi, Fadlu Davids amewahi kufundisha timu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Orlando Pirates, Maritzburg United, na Cape Town City. Pia amewahi kuwa kocha msaidizi katika klabu za Raja Casablanca ya Morocco na Lokomotiv Moscow ya Urusi.
Ifuatayo ni orodha ya timu na nafasi alizoshikilia, pamoja na kipindi alichohudumu:
Klabu & Nafasi | Kuteuliwa | Alihudumu Hadi |
Raja Casablanca – Kocha Msaidizi | 23/24 (Jul 1, 2023) | – |
Maritzburg Utd. – Meneja | 22/23 (Nov 14, 2022) | 23/24 (Jun 30, 2023) |
Loko Moscow – Kocha Msaidizi | 22/23 (Sep 27, 2022) | 22/23 (Oct 9, 2022) |
Orlando Pirates – Meneja | 21/22 (Aug 17, 2021) | 21/22 (Jun 30, 2022) |
Orlando Pirates – Kocha Msaidizi | 18/19 (Jan 15, 2019) | 21/22 (Aug 16, 2021) |
Maritzburg Utd. – Meneja | 17/18 (Jul 1, 2017) | 18/19 (Dec 24, 2018) |
Maritzburg Utd. – Meneja wa Muda | 16/17 (Mar 23, 2017) | 16/17 (Jun 30, 2017) |
Maritzburg Utd. – Kocha Msaidizi | 16/17 (Jan 10, 2017) | 16/17 (Mar 22, 2017) |
Maritzburg Utd. – Meneja wa Muda | 16/17 (Nov 24, 2016) | 16/17 (Jan 9, 2017) |
Maritzburg Utd. – Kocha Msaidizi | 15/16 (Dec 28, 2015) | 16/17 (Nov 24, 2016) |
Maritzburg Utd. – Meneja wa Muda | 15/16 (Dec 1, 2015) | 15/16 (Dec 27, 2015) |
Maritzburg Utd. – Kocha Msaidizi | 15/16 (Sep 25, 2015) | 15/16 (Nov 30, 2015) |
Maritzburg Utd. – Meneja wa Muda | 15/16 (Sep 15, 2015) | 15/16 (Sep 24, 2015) |
Maritzburg Utd. – Kocha Msaidizi | 15/16 (Jul 2, 2015) | 15/16 (Sep 14, 2015) |
Chippa United – Kocha Msaidizi | 14/15 (Jan 7, 2015) | 14/15 (Jun 30, 2015) |
B.Fontein Celtic – Kocha Msaidizi | 13/14 (Jan 13, 2014) | 14/15 (Dec 15, 2014) |
Maritzburg Utd. – Kocha Msaidizi | 12/13 (Jul 1, 2012) | 13/14 (Jan 12, 2014) |
Mapendekezo ya Mhariri:
- CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025
- Cv Ya Steven Mukwala Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025
- Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba
- Yanga Yampa Farid Mussa Mkataba wa Miaka Miwili Zaidi
- Yanga Yafukuzisha Kocha Mamelodi Sundowns
- Jean Charles Ahoua Kurithi Mikoba ya Chama Simba 2024/2025
- Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Dirisha la Usajili Ligi Kuu Tanzania kufunguliwa Juni 15 hadi Agosti 15, 2024
Weka Komenti