Fei Toto Aweka Wazi Nia ya Kuvaa Jezi Nyekundu ya Al Ahly
Kiungo mshambuliaji mahiri wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto,’ ameibua gumzo jipya katika mitandao ya kijamiina kwa mashabiki wengi wa soka Tanzania baada ya kuweka wazi ndoto yake ya kucheza soka la kulipwa katika klabu kubwa barani Afrika, Al Ahly ya Misri. Je, hii inaashiria mwanzo wa safari mpya kwa nyota huyu anayekuja kwa kasi?
Fei Toto Aweka Wazi Nia ya Kuvaa Jezi Nyekundu ya Al Ahly
Katika mahojiano ya hivi karibuni, Fei Toto hakusita kufichua ndoto yake ya kuvaa jezi nyekundu ya Al Ahly, klabu yenye historia ndefu ya mafanikio makubwa katika soka la Afrika. Ameeleza kuvutiwa na heshima kubwa ambayo Al Ahly imejiwekea katika soka la bara hili, pamoja na makombe mengi waliyoshinda ndani na nje ya Misri.
“Al Ahly ni klabu kubwa sana Afrika,” Fei Toto alisema. “Historia yao inajieleza yenyewe. Ningependa sana kupata nafasi ya kucheza katika kiwango hicho cha juu na kuchangia mafanikio ya klabu.”
Je, Fei Toto Anasifa za Kujiunga Al Ahly?
Fei Toto amekuwa mmoja wa wachezaji wanaong’ara zaidi katika Ligi Kuu Tanzania Bara, akiwa na uwezo mkubwa wa kufunga magoli haswa akiwa nje ya boksi na kutoa pasi za mwisho zenye madhara. Ustadi wake wa kucheza katika nafasi tofauti za ushambuliaji na hata ukabaji unamfanya kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa kwa timu yoyote, na hii imejidhihirisha baada ya kujiunga na Azam akitokea Yanga Sc ambapo mchango wake hauhitaji utambulisho wowote kwa yeyote mwenye uelewa na mchezo wa soka.
Je, Al Ahly watavutiwa na kipaji cha Fei Toto?
Kuna uwezekano mkubwa kwa mabingwa wa klabu bingwa Afrika Al Ahly kuwa ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya nyota huyu wa Tanzania. Ikiwa Fei Toto ataendelea kung’ara katika kiwango chake cha sasa hasa katika michuano ya CAF 2024/2025 ambayo atashiriki akiwa ndani ya jezi ya Azam Fc, huenda ndoto yake ya kucheza Misri ikaanza kutimia.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Hizi Apa Takwimu za Stephane Aziz Ki na Feisal Salum 2023/2024
- Yanga Yafanikiwa Kutetea Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB 2024
- Kanuni Mpya za Mfungaji Bora Ligi Kuu Ya NBC Tanzania 2023/2024
- Ni Yanga Vs Azam Fainali Ya Kombe La Shirikisho (CRDB Federation Cup)
- Timu Zilizofuzu UEFA Champions League 2024/2025
- Vinara wa Assist Ligi Kuu NBC 2023/24: Wafalme wa Pasi za Mwisho Tanzania
- Orodha Ya Wafungaji Bora Ligi Kuu Ya NBC Tanzania 2023/2024
- Magoli Mawili ya Haaland Yarejesha Man City Kileleni mwa Msimamo wa Ligi
- List Ya Wachezaji Wenye Magoli Mengi Duniani
Weka Komenti