Takwimu za Stephane Aziz Ki na Feisal Salum 2023/2024: Hizi Apa Takwimu za Stephane Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum wa Azam FC msimu wa 2023/2024 Ligi Kuu Ya NBC Tanzania
Msimu wa 2023/2024 bila shaka umekua msimu mzuri kwa kwa Stephane Aziz Ki na Feisal Salum. Wote wameonyesha kiwango cha hali ya juu, wakiongoza klabu zao kwa umahiri mkubwa. Lakini, takwimu zinasemaje kuhusu nyota hawa wawili? Hizi hapa takwimu za motomoto kueleke kinyang’anyiro cha kuwania kiatu cha mfungaji bora ligi kuu Tanzani.
Hizi Apa Takwimu za Stephane Aziz Ki na Feisal Salum 2023/2024
Mchezaji | Aziz Ki | Feisal |
Mechi | 23 | 26 |
Dakika | 1,814 | 2172 |
magoli | 15 | 15 |
Hattrick | 1 | 1 |
Asisti | 8 | 7 |
Penalti | 2 | 1 |
Katika msimu huu, Aziz Ki amecheza jumla ya mechi 23, huku Feisal Salum akiwa na mechi 26 chini ya ukanda wake. Ingawa Feisal amecheza mechi zaidi, Nyota wa Yanga Sc Aziz Ki ameonekana kuwa na takwimu nzuri kumzidi Feisal salum wa Yanga ambae amecheza dakika 2172 tofauti za 1814 ambazo amecheza Aziz Ki.
Linapokuja suala la ufungaji, wachezaji hawa wameonesha umahiri mkubwa. Kila mmoja ameweza kufunga magoli 15 katika msimu huu, huku wote wakiweza kufunga hat trick moja. Hii inaonyesha uwezo wao wa kipekee wa kubeba mzigo wa ufungaji kwa timu zao.
Kando na kufunga magoli, wachezaji hawa pia wameonesha ujuzi wao katika kutoa pasi za mwisho. Aziz Ki ametoa jumla ya asisti 8, wakati Feisal Salum ametoa asisti 7 kwa wenzao uwanjani. Hii inaonyesha uwezo wao wa kufanya kazi kama timu na kusaidia timu zao kupata matokeo mazuri.
Katika eneo la penalti, Aziz Ki ameonesha utaalamu wake kwa kufunga penalti 2, huku Feisal Salum akifunga moja. Uwezo wao wa kutumia nafasi hizi muhimu za kufunga magoli unathibitisha umahiri wao na kujiamini uwanjani.
Kwa jumla, takwimu hizi zinaonyesha jinsi Stephane Aziz na Feisal Salum walivyochangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya vilabu vyao katika msimu wa 2023/2024. Uwezo wao katika kufunga magoli, kutoa pasi za mwisho, na hata katika kutekeleza penalti, unawafanya kuwa nguzo muhimu katika timu zao. Tutabaki kufuatilia kwa hamu mafanikio yao katika misimu ijayo ya soka!
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti