Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
Katika ulimwengu wa mawasiliano wa leo, kuwa na salio la kutosha kwenye simu yako ni muhimu kwa kuwasiliana na ndugu, marafiki, na wafanyakazi wenzako. Lakini vipi kama salio lako litaisha ghafla na unahitaji kupiga simu muhimu au kutuma ujumbe wa dharura? Mtandao wa Airtel unatoa suluhisho la haraka kupitia huduma yake ya “kukopa salio,” inayojulikana kama Daka Salio.
Huduma ya Airtel Daka salaio inaruhusu wateja wa Airtel kukopa kiasi kidogo cha salio la muda wa maongezi ili kukidhi mahitaji yao ya haraka. Huduma hii ni rahisi kutumia na inaweza kuwa mkombozi katika hali zisizotarajiwa ambapo salio lako la kawaida limeisha.
Kama wewe ni mtumiaji mpya wa Airtel au ni mteja wa Airtel ambaye hujawahi kutumia huduma ya Airtel daka salio na ungependa kufahamu jinsi ya kutumia huduma hii, basi sisi Habariforum.com tutakujuza jinsi ya kukopa salio Airtel kiurahisi.
Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
Kukopa Salipo Airtel Piga h *149*44#
Vigezo Na Masharti Ya Huduma Ya Airtel Daka Salio
- Huduma hii kitakuwa kinapatikana kwa wateja wa malipo ya kabla
- Huduma hii iitakuwa inapatikana kupitia *149*44 # menyu ya huduma.
- Mtumiaji lazima awe kwenye mtandao wa Airtel kwa angalau siku 90.
- Mtumiaji atalipa ada ya huduma ya 15% kwa ajili ya huduma ya mkopo.
- Ada ya huduma ya 15% inakusanywa wakati wa kuongeza salio.
- Mtumiaji ataomba mkopo, atapokea muda wa maongezi au kifurushi cha kiasi kilichoombwa.
- Mchakato wa ulipaji wa mkopo hutokea wakati mtumiaji anaongeza muda wa maongezi ambapo kiasi cha mkopo kitaondolewa kwanza na salio lilibaki litawekwa katika akaunti kuu ya mtumiaji.
- Mkopo lazima kulipwa baada ya siku 7.
- Airtel haitofidia kwa huduma yoyote iliyonunuliwa. Vifurushi vyote vilivyonunuliwa lazima vitumike kama ilivyoekezwa katika menyu ya huduma.
- Airtel Tanzania PLC ina haki ya kusahihisha au kurekebisha vigezo hivi na masharti au kuondoa bidhaa wakati wowote. Tukio lolote katika hayo, taarifa itakuwa na ufanisi mara moja au kama tarehe ilivyotajwa katika arifu kama hizo.
Mapendekezo Ya Mhariri: Jinsi ya Kukopa Salio Tigo (Menu Ya Kukopa Salio Tigo) 2024
Weka Komenti