Kikosi Cha Yanga Vs FC Augsburg Mpumalanga Cup 20/July/2024 | Kikosi cha Yanga Dhidi ya Augsburg
Klabu ya Yanga Sc itakutana na wababe wa soka kutoka ujerumani FC Augsburg katika mchezo ambao bila shaka utaenda kuandikwa katika vitabu vya historia ya soka nchini Tanzania. Mchezo huu utakua ni mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Mpumalanga Premier international Cup 2024 ambayo inafanyika Afrika Kusini. Katika mchezo huu, Yanga Sc inatarajiwa kuonesha makali ya kikosi chake baada ya kukifanyia maboresha kwa kuongeza nyota mbalimbali lakini mkubwa zaidi ni Chama kutoka Simba.
Chama amejiunga na klabu ya Yanga akitokea SImba na kipaji chake kinajulikana kwa kila shabiki wa mpira. Je uwepo wa Chama, Aziz Ki, Pacome na Max utaisaidia Yanga Kuandika historia mpya kwa kuwashushia kipongo FC Augsburg ya ujerumani? Au ni mabingwa wa ujerumani wataifundisha Yanga namna ya kulisakata kabumbu!? Hapa tumekuletea utabiri wa kikosi cha Yanga Sc dhidi ya FC Augsburg wakati tukisubiri kikosi rasmi kitakacho tangazwa na Kocha wa Yanga Sc Miguel Ángel Gamondi.
Taarifa Kuhusu Mechi
🏆 #MpumalangaCup🇿🇦
⚽️ FC Augsburg🇩🇪🆚Young Africans SC🇹🇿
📆 20.07.2024
🏟 Mbombela Stadium
🕖 15H00🇿🇦
Kikosi Cha Yanga Vs FC Augsburg Mpumalanga Cup 20/July/2024
RASMI; Kocha wa Yanga ametangaza kikosi cha Yanga kitakacho cheza mechi ya leo dhidi ya FC Augsburg kwenye mechi ya Mpumalanga Cup. Hapa tumekuletea kikosi rasmi kilichotangawa na Miguel Ángel Gamondi
- 39 Diarra
- 21 Yao
- 30 Kibabage
- 5 D. Job
- 4 Bacca
- 18 Sureboy
- 7 Maxi
- 27 Mudathir
- 24 Clement
- 17 Chama
- 10 Aziz Ki
Substitutes
- Khomeny
- Mwamnyeto
- Aziz A.
- Boka
- Mkude
- Duke
- Shekhan
- Dube
- Baleke
ANGALIA: Matokeo ya Yanga vs FC Augsburg Leo 20 Julai 2024: Yaliyojiri Uwanjani
Kocha Miguel Ángel Gamondi amekuwa akifanya kazi kwa karibu na wachezaji wake ili kuhakikisha wanakuwa tayari kwa mchezo huu muhimu. Kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kuanza dhidi ya FC Augsburg kinaweza kuwa kama ifuatavyo:
Mlinda Lango: Diarra
Mabeki: Yao, Job, Bacca, Boka
Viungo: Aucho, Pacome, Nzengeli, Aziz Ki, Chama
Mshambuliaji: Dube
Kocha: Miguel Ángel Gamondi.
Je, Chama Atafanya Maajabu?
Kipaji cha Chama kinasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Yanga. Akiwa na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali za kiungo na mshambuliaji, uwepo wake unaweza kuleta tofauti kubwa dhidi ya mabingwa wa Ujerumani. Mashabiki wana matumaini makubwa kuwa Chama ataweza kuisaidia Yanga kufanikisha ushindi dhidi ya FC Augsburg.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mpumalanga Premier international Cup 2024
- Ratiba ya Mechi Zijazo za Yanga 2024/2025
- Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025
- Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
- Rekodi za Simba na Yanga Kufungana
- Wafungaji Bora CECAFA Dar Port Kagame Cup 2024
- Timu Zinazoshiriki Mpumalanga Premier International Cup 2024
- Cv ya Awesu Ali Awesu Kiungo Mpya Simba 2024/2025
Weka Komenti