Matokeo ya Simba Vs APR Leo 03 Agosti 2024 – Simba Day | Matokeo ya Simba Dhidi ya APR FC Leo Mechi ya Kirafiki
Klabu ya Simba leo itachuana na wageni wao APR FC katika mchezo wa kirafiki ambao ni sehemu ya sherehe ya Simba Day.
Mchezo huu utapigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ukiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 88 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo yenye makazi yake Kariakoo, Ilala.
APR FC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Rwanda, walifika jijini Dar es Salaam asubuhi ya Ijumaa, Agosti 2, wakiwa na kikosi cha wachezaji 24. Kati ya hao, kuna wachezaji 10 wapya waliojiunga na timu msimu huu, akiwemo Lamine Bah kutoka Mali, pamoja na Wanaigeria Johnson na Odibo.
Baadhi ya wachezaji wa APR FC waliokosa safari ni Nshimirimana Ismael Pichou, Apam Bemol ambaye alipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza, na Kwitonda Alain Bacca ambaye hajaonyesha uwezo wa kumvutia kocha.
Aidha, kipa wa tatu Ivan Ruhamyankiko naye hakusafiri. APR FC iliwahi kucheza Tanzania Julai 21, 2024, ambapo walipoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame CECAFA dhidi ya Red Arrows.
Hii itakuwa fursa nyingine kwa APR FC kujipima nguvu dhidi ya timu kubwa ya Simba kabla ya kuelekea mechi yao ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Azam FC itakayofanyika Agosti 18 kwenye uwanja wa Compex Chamazi.
Matokeo ya Simba Vs APR Leo 03 Agosti 2024 – Simba Day
Ingawa ni mchezo wa kirafiki, mchezo wa leo kati ya Simba na APR unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa. Timu zote mbili zina wachezaji wenye vipaji na zina hamu ya kushinda mchezo huu kwa lengo la kuwapa mashabiki furaha.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania na Rwanda watakuwa na hamu ya kuona ni timu gani itaibuka kidedea katika mtanange huu wa kusisimua. Hapa tutakuletea taarifa za moja kwa moja kutoka katika dimba la Benjamin mkapa mara baada ya mchezo kuanza.
Angalia Hapa Select Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 – Simba Day
Simba SC | 2-0 FT | APR FC |
- Dakika 20 za mchezo zimepita bila kufungana: Simba 0-0 APR FC
- Dakika ya 43, Simba wanapata penati baada Mutale kuchezewa faulo kwenye boksi
- Mkwala anakosa penati. Dakika ya 44 Simba 0-0 APR FC
Stev Mukwala anakosa penati hapa !! pic.twitter.com/2yrneJQhNU
— SportsArenaTz (@SportsarenatzTz) August 3, 2024
- Kipindi cha Kwanza Kimeisha; Simba 0-0 APR FC
- Dakika ya 46 Debora Fernandez anaifungia Simba goli la kuongoza
- Dakika ya 66 Balua anaifungia Simba goli la pili
Katika mchezo huu wa kirafiki, Simba SC watajaribu kuonyesha uwezo wao dhidi ya mabingwa wa Rwanda, APR FC, kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa. Tukio hili linatarajiwa kuwa na burudani kubwa, likiimarisha uhusiano kati ya klabu na mashabiki huku likiashiria mwanzo mpya wa mafanikio kwa Simba SC.
Simba Day: Zaidi ya Mpira, Ni Sherehe ya Utamaduni
Simba Day ni tukio kubwa kwa klabu ya Simba, likifanyika kila mwaka na kujumuisha mashabiki wengi wanaofika kusherehekea mafanikio ya klabu yao. Mwaka huu, tukio hilo limevuta hisia nyingi, ambapo mashabiki 60,000 wanatarajiwa kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa.
Wiki ya Simba ilianza Julai 24, ikijumuisha shughuli mbalimbali za kijamii kama vile michango ya damu na misaada kwa wenye mahitaji maalum, kuonyesha kujali jamii na kujitolea kwa klabu hiyo.
Kabla ya Simba Day, Simba walikuwa na mechi za kirafiki nchini Misri wakijaribu kuboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu mpya.
Msimu uliopita, Simba walipata changamoto nyingi, wakitolewa katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Al Ahly, na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Simba ina matumaini makubwa kwa msimu ujao kutokana na maandalizi makubwa na usajili mpya wa wachezaji. Sherehe za Simba Day zitakuwa fursa ya kutambulisha wachezaji wapya na kuleta mshikamano zaidi kati ya klabu na mashabiki wake.
Mashabiki wa Simba wanasubiri kwa hamu kubwa matukio na sherehe zilizopangwa kwa ajili ya Wiki ya Simba na Simba Day, wakitarajia kuona timu yao ikirudi kwenye ubora wake na kufanikiwa zaidi katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya Rayon Sports Vs Azam Fc Leo Agosti 03 2024
- Orodha ya Makocha Timu za Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
- Kikosi Cha Azam Fc Vs Rayon Sports Agosti 03 2024
- Kibu Denis Arejea Simba SC Huku Akisubiri Uamuzi wa Kamati ya Nidhamu
- Meddie Kagere Aongezewa Mkataba Wa Mwaka Mmoja Namungo FC
- Cv Ya Moussa Camara Kipa Mpya Wa Simba 2024/2025
Weka Komenti