Cv Ya Moussa Camara Kipa Mpya Wa Simba 2024/2025

Cv Ya Moussa Camara Kipa Mpya Wa Simba 2024/2025

Klabu ya Simba SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2024/2025 ambao unatarajiwa kuanza Agosti 8 kwa michezo ya Ngao ya jamii. Katika juhudi za kuendelea kuboresha kikosi, Simba Sc imetangaza kumsaji Moussa Camara, raia wa Guinea. Camara mwenye umri wa miaka 25 amejiunga na kikosi cha Wekundu wa Msimbazi akitokea klabu ya Horoya Athletic Club. Usajili wake unalenga kuimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo kuelekea msimu wa 2024/2025.

Wasifu wa Moussa Camara

Moussa Camara ni mlinda mlango ambaye ameonyesha umahiri mkubwa katika michezo mbalimbali akiwa na klabu yake ya zamani. Hapa chini ni wasifu wake wa kina:

Taarifa Binafsi

Taarifa Maelezo
Tarehe ya kuzaliwa/Umri Novemba 27, 1998 (Miaka 25)
Mahali pa kuzaliwa Siguiri, Guinea
Urefu 1,85 m
Uraia Guinea
Nafasi Kipa
Wakala wa Mchezaji Sifeza Sports
Klabu ya sasa Simba SC
Aliyijiunga Agosti 01, 2021

Cv Ya Moussa Camara Kipa Mpya Wa Simba 2024/2025

Safari ya Soka Moussa Camara Kipa Mpya Wa Simba

Moussa Camara alianza safari yake ya soka katika klabu za vijana nchini Guinea na kisha kujiunga na Milo Fc Julai 1, 2014, ambapo alidumy hadi Dec 1, 2015 kisha kujiunga na Horoya Athletic Club. Akiwa na Horoya, alifanikiwa kuonyesha uwezo mkubwa wa kudaka mpira, jambo lililomfanya kujulikana zaidi kwenye soka la kimataifa.

Moussa Camara amejiunga na Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili. Ujio wake unaleta matumaini makubwa kwa klabu hiyo kutokana na uwezo wake wa hali ya juu wa kulinda lango. Camara ameshukuru uongozi wa Simba kwa kumpa nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi hicho na ameahidi kufanya vizuri ili kuisaidia timu hiyo kufikia malengo yake.

Hitimisho

Usajili wa Moussa Camara katika klabu ya Simba SC ni hatua muhimu katika kuimarisha kikosi kuelekea msimu mpya wa 2024/2025. Uwezo wake wa kudaka na kuokoa michomo, pamoja na kujiweka vizuri golini, ni faida kubwa kwa Simba. Hata hivyo, anapaswa kuendelea kujitahidi kuboresha maeneo yenye udhaifu ili aweze kuwa kipa bora zaidi.

Simba SC inatarajia mafanikio makubwa kutoka kwa Camara, na mashabiki wana matumaini makubwa kuwa atasaidia klabu hiyo kutwaa mataji mbalimbali msimu ujao.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Cv ya Awesu Ali Awesu Kiungo Mpya Simba 2024/2025
  2. Cv ya Karaboue Chamou Beki Mpya Wa Simba 2024/2025
  3. Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba
  4. CV ya Valentin Nouma: Sifa Zote za Beki Mpya Simba 2024/2025
  5. CV ya Fadlu Davids: Kocha Mpya wa Simba SC (2024/2025)
  6. Cv YA Boka Chadrak Beki Mpya Wa Yanga 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo