Matokeo ya Uhamiaji vs Al Ahli Tripoli Leo 18/08/2024 | Matokeo ya Uhamiaji Fc Leo Dhidi ya Al Ahli
Leo tarehe 18 Agosti 2024, klabu ya Uhamiaji ya Zanzibar itashuka dimbani dhidi ya Al Ahli Tripoli kutoka Libya katika mechi ya hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mechi hii itachezwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Tripoli, jijini Tripoli, na itaanza saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, badala ya saa 9:30 alasiri kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Timu ya Uhamiaji imepata nafasi ya kushiriki michuano hii baada ya Chipukizi ya Pemba, ambao walikuwa washindi wa Kombe la Shirikisho (ZFF), kujitoa kushiriki kutokana na changamoto za kiuchumi. Hali hii iliwalazimu maafande wa Uhamiaji kuchukua nafasi hiyo na kukubali kucheza mechi zao zote za hatua ya awali jijini Tripoli kama ilivyoamuliwa kwa JKU.
Kwa Uhamiaji, hii ni mara ya kwanza kuwakilisha Zanzibar kwenye michuano ya kimataifa, na wanakabiliwa na mtihani mkubwa dhidi ya Al Ahli Tripoli, timu ambayo ina historia ya mafanikio katika soka la Libya na kanda ya Kaskazini mwa Afrika.
Uhamiaji inakutana na Al Ahli Tripoli katika kipindi muhimu ambapo watahitaji kuonyesha uwezo wa hali ya juu ili kusonga mbele katika michuano hii. Mechi ya leo ni ya kwanza kati ya mbili zitakazochezwa, na matokeo ya leo yatakuwa na umuhimu mkubwa katika kuamua hatma yao. Mchezo wa marudiano pia utafanyika jijini Tripoli wiki ijayo, ambapo mshindi wa jumla ataweza kukutana na Simba SC katika raundi ya pili.
Kwa Uhamiaji, hii ni nafasi adimu ya kuonesha uwezo wao katika anga za kimataifa, huku wakiwa na jukumu zito la kutetea heshima ya Zanzibar. Ushiriki wao katika michuano hii ni ishara ya maendeleo ya soka la Zanzibar, na mafanikio dhidi ya timu kama Al Ahli Tripoli yanaweza kuwa chachu ya maendeleo zaidi.
Matokeo ya Uhamiaji vs Al Ahli Tripoli Leo 18/08/2024
Uhamiaji | VS | Al Ahli Tripoli |
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha JKU Vs Pyramids Leo 18/08/2024 CAF
- Matokeo Ya JKU Vs Pyramids Leo 18/08/2024 Klabu Bingwa
- Kikosi Cha Azam Vs APR Leo 18/08/2024 Club Bingwa
- Matokeo ya Azam Vs APR Leo 18/08/2024 Klabu Bingwa
- Kikosi cha Kengold 2024/2025 (Wachezaji wote wa KenGold FC)
- Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
Weka Komenti