Matokeo ya Azam Vs APR Leo 18/08/2024 Klabu Bingwa | Matokeo ya Azam Leo Dhidi ya APR CAF Champions
Leo hii, tarehe 18 Agosti 2024, Wana ramba ramba Azam FC wanakabiliwa na changamoto kubwa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika hatua ya awali. Timu hii, iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu uliopita, itakutana na mabingwa wa Rwanda, APR FC, katika dimba la Azam Complex. Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12:00 jioni na unakuwa ni hatua muhimu kwa Azam FC kurejea kwa kishindo katika michuano ya Afrika.
Azam FC imefanikiwa kurejea tena kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuikosa kwa muda mrefu. Mara ya kwanza kushiriki ilikuwa mwaka 2015 baada ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013-2014. Msimu huo, Azam FC ilijivunia rekodi ya kushinda michezo 18 na kutoka sare katika michezo 8 kati ya 26, chini ya Kocha Mcameroon, Joseph Omog.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Azam FC kushiriki katika michuano hii, na matarajio ya klabu ni kufika mbali zaidi, hasa katika hatua ya makundi. Kocha wa Azam FC ameweka wazi malengo ya timu kwa msimu huu, akisisitiza umuhimu wa kutumia vyema uwanja wa nyumbani kabla ya mechi ya marudiano itakayofanyika Kigali, Rwanda, Agosti 24, 2024.
APR FC, mabingwa mara 22 wa Ligi Kuu Rwanda, wanakuja Tanzania wakiwa na historia na nguvu kubwa katika michuano ya kikanda. Timu hii imeshiriki michuano kadhaa ya kujiandaa kwa msimu huu, ikiwemo Kombe la Kagame lililofanyika jijini Dar es Salaam. Katika fainali ya Kombe hilo, APR ilipoteza kwa mikwaju ya penalti 10-9 dhidi ya Red Arrows ya Zambia baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Aidha, APR pia ilicheza dhidi ya Simba SC katika tamasha la ‘Simba Day’ lililofanyika Agosti 3, 2024, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo, APR ilifungwa mabao 2-0, lakini matokeo hayo hayaondoi ukweli kwamba APR ni timu yenye uwezo mkubwa, na mchezo wa leo dhidi ya Azam FC unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa.
Matokeo ya Azam Vs APR Leo 18/08/2024 Klabu Bingwa
Azam Fc | 1-0 | APR FC |
- AZAM VS APR FC
- 🏆 Klabu Bingwa Africa CAF
- ®️ 1ST Preliminary Round
- 🏟 Azam Complex
- 🕰 6.00 PM (E.A.T)
Mchezo huu wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, kutokana na maandalizi ya timu zote mbili. Azam FC, ikiwa na faida ya kucheza nyumbani, inatarajiwa kutumia kikamilifu nafasi hiyo ili kupata matokeo mazuri kabla ya kuelekea kwenye mchezo wa marudiano. Kwa upande mwingine, APR FC wanakuja wakiwa na lengo la kupata matokeo mazuri ugenini ili kurahisisha kazi nyumbani kwao.
Mashabiki wa Azam FC na wapenzi wa soka nchini Tanzania wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao, na matumaini ni kwamba Azam FC itaweza kuwakilisha vyema nchi katika michuano hii muhimu ya Afrika.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti