Simba SC Yatoa Tamko Rasmi Kuhusu Kibu Mkandaji
Katika hali inayoacha mashabiki wa soka vinywa wazi, Simba SC, moja ya klabu kongwe na maarufu nchini Tanzania, imetoa tamko rasmi kuhusu mchezaji wao, Kibu Denis Prosper, maarufu kama “Kibu Mkandaji.” Tamko hili limekuja baada ya mchezaji huyo kutoonekana kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara 2024/25, jambo ambalo limeibua wasiwasi na uvumi mwingi miongoni mwa mashabiki wa klabu ya Simba Sc na wadau mbalimbali wa soka.
Simba SC, kupitia kurasa zao za mitandano ya kijamii, imesema kuwa Kibu Mkandaji hajafika kambini kwa muda mrefu na hajawasilisha sababu zozote za kutokuwepo kwake. Klabu imeeleza kuwa kitendo hicho ni utovu wa nidhamu na kinyume na mkataba wake na klabu.
Hatua Kali za Kinidhamu Zatarajiwa
Klabu ya Simba SC imesema kuwa itamchukulia hatua kali za kinidhamu Kibu Mkandaji kwa mujibu wa kanuni na taratibu za klabu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Hatua hizo zinaweza kujumuisha faini, kusimamishwa kucheza, au hata kuvunja mkataba wake. Baada ya tamko hili, mustakabali wa Kibu Mkandaji ndani ya Simba SC umekuwa mashakani. Mchezaji huyo ambaye alikuwa tegemeo kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba katika msimu wa 2023/2024, sasa anakabiliwa na uwezekano wa kuondoka klabuni hapo kwa njia isiyo nzuri.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo Simba Vs El-Qanah Egypt Leo (22 July 2024) Mechi Ya Kirafiki
- Kikosi cha Simba Vs El-Qanah Egypt Mechi Ya Kirafiki (22 July 2024)
- Awesu na Onana Watua Misri Kujiunga na Kambi ya Mazoezi ya Simba
- Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025
- Rekodi za Simba na Yanga Kufungana
- Jezi Mpya za Simba 2024/25
- Cv ya Awesu Ali Awesu Kiungo Mpya Simba 2024/2025
Weka Komenti