Klabu ya Simba Sc Yafunga Safari Kuifata kagera Sugar kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania.
Klabu ya Simba Sc imefunga safari kutokea jijini Dar es alaam kuelekea Kagera kuifata kagera sugar kwa ajili ya mechi ya Ligi kuu ya NBC Tanzania 2023/2024 itakayochezeka may 12 2024 katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Simba Sc Yafunga Safari Kuifata kagera Sugar
Mchezo huu utakua mchezo wa 26 kwa mabingwa wa soka mitaa ya Kariakoo uku katika michezo 25 ambayo wameshakwisha cheza, wameweza kushinda mechi 17, kutoa sare mechi 5 na kufungwa mechi 3. Hadi sasa simba wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya NBC wakiwa wamezidiwa pointi moja na Azam wenye jumla ya points 56 baada ya kucheza mechi 26.
Mechi ya Simba Sc Vs Kagera sugar ni mechi yenye uzito mkubwa kwa klabu ya Simba Sc sababu ndiyo itaamua kama Simba Sc watashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kujihakikishia ushiriki kwenye michuano ya CAF champions league kwa mwaka 2024/2025
Kwa upande wa wenyeji wa Simba Sc, Kagera Sugar wanashikiria nafasi ya 9 wakiwa na jumla ya pointi 26 walizozikusanya katika michezo 26 ya ligi uku wakiwa wameweza kushinda michezo 6, kutoa sare mara 12 na kupoteza michezo 8.
Maneno ya Kocha Wa Simba Sc Kuelekea Mchezo Wao Dhidi ya Kagera Sugar
Kocha Mgunda kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar.
Taarifa zaidi kwenye Simba App. #WenyeNchi #NguvuMoja pic.twitter.com/4YAc4qtrjp
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) May 11, 2024
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti