Ley Matampi Golikipa mwenye Clean Sheet Nyingi Ligi Kuu NBC 2023/2024 | Ley Matampi Aongoza kuwa na mechi nyingi bila kufungwa ligi kuu ya NBC Tanzania 2023/2024
Ley Matampi Golikipa mwenye Clean Sheet Nyingi Ligi Kuu NBC 2023/2024
Ligi Kuu ya NBC Tazania msimu wa 2023/2024 imemalizika uku ikiwa imeshuhudia ushindani wa hali ya juu katika kila nyanja, na miongoni mwa nyota wapya waliojitokeza kung’ara ni Ley Matampi, golikipa mahiri wa Coastal Union FC. Matampi ameibuka mshindi wa tuzo ya “Golden Gloves” kwa kuweka rekodi ya clean sheet 15, akiwaacha nyuma makipa wengine mahiri kama Djigui Diarra wa Yanga.
Matampi alijiunga na Coastal Union akitokea Jeunesse Sportive Groupe Bazano ya DR Congo, na kwa haraka akaonyesha umahiri wake. Akiwa na urefu wa kutosha, uwezo wa kuongoza safu ya ulinzi, na mikono ya sumaku, Matampi aliibuka kuwa tishio kwa washambuliaji wa timu pinzani. Clean sheet zake 15 sio tu zilimpa tuzo ya kibinafsi, bali pia zilichangia pakubwa mafanikio ya Coastal Union kumaliza katika nafasi ya nne kwenye ligi na kufuzu kwa Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Mafanikio ya Matampi yamevutia hisia za vilabu vikubwa, ikiwemo Simba SC, ambao wanaripotiwa kumnyatia kwa ajili ya msimu ujao.
Mpinzani wa Karibu: Djigui Diarra
Djigui Diarra wa Yanga, aliyewahi kushinda tuzo ya “Golden Gloves” miaka miwili mfululizo, alitoa upinzani mkali kwa Matampi. Akiwa amemaliza msimu wa ligi kuu ya NBC na clean sheet 14, Diarra alionyesha uwezo wake mkubwa licha ya Yanga kubeba ubingwa wa ligi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Timu za Tanzania Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Timu Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Muonekano wa Kombe La CRDB Federation Cup 2023/2024
- Harry Kane Ndio Mshindi wa Kiatu cha Dhahabu Ulaya 2023-2024
- Timu Inayoongoza kwa Magoli Ligi Kuu Ya NBC 2023/2024
- Timu zilizopanda Daraja Ligi Kuu ya England EPL 2024/2025
- Picha Za Parade ya Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24
Weka Komenti