Matokeo ya Vitalo Vs Yanga Leo 17/08/2024 CAF Champions League | Matokeo ya Yanga Klabu Bingwa Leo | Matokeo ya Vitalo Vs Yanga Leo Mechi ya klabu bingwa Afrika
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC Tanzania na Ngao ya Jamii Yanga Sc leo wanatarajia kuanza rasmi safari yao ya michuano ya kimataifa CAF ambapo watachuana na klabu ya Vital’o ya Burundi. Mchezo huu utaanza majira ya kumi jioni katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi na unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa na mvuto wa aina yake.
Kocha Mkuu wa Vitalo FC, Sahabo Parris, ameweka wazi kuwa kikosi chake kimefanya maandalizi ya kutosha kukabiliana na Yanga SC katika mchezo huu muhimu wa Klabu Bingwa Afrika.
Licha ya kuwaheshimu Yanga SC kama timu yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa, Parris amesisitiza kuwa hakuna mechi rahisi katika mashindano haya ya ngazi ya juu barani Afrika. Vital’O FC, yenye historia ndefu na mafanikio makubwa nchini Burundi, ikiwemo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka wa 1992, inaingia uwanjani ikiwa na matumaini ya kupata matokeo mazuri dhidi ya Yanga.
Kwa upande wao, Yanga SC, kupitia kwa Ofisa Habari wao Ali Kamwe, wameonyesha kujiamini kuelekea mchezo huu.
Kamwe amebainisha kuwa Yanga SC inakwenda uwanjani ikiwa tayari kupambana na kuonyesha ubora wao kwa vitendo, licha ya tambo za wapinzani wao. Wachezaji wote muhimu wa Yanga, wakiwemo Clatous Chama, Aboutwalib Mshery, Djigui Diarra, Sure Boy, Aziz Ki, Farid Mussa, Maxi Nzengeli na Pacome, wapo fiti na tayari kwa mchezo huu.
Matokeo ya Vitalo Vs Yanga Leo 17/08/2024 CAF
Vital’o | 0-4 FT | Yanga |
|
- 🏆 #Klabu Bingwa Afrika
- ⚽️ Vital’O FC🆚Young Africans SC
- 📆 17.08.2024
- 🏟 Azam Complex
- 🕖 Saa Kumi Jioni
Mchezo huu wa leo ni wa kwanza kati ya miwili ya hatua ya awali ya Ligi ya klabu bingwa Afrika. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Agosti 24, 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mshindi wa jumla wa mechi hizi mbili atakutana na mshindi kati ya Commercial Bank of Ethiopia na Sports Club Villa ya Uganda katika raundi inayofuata.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ifahamu Timu ya Vital’O Mpinzani wa Yanga CAF Champions league
- KMC na Simba Wafikia Makubaliano ya Uhamisho wa Kiungo Awesu Awesu
- Ahmed Arajiga Ateuliwa na CAF Kuchezesha Mechi ya Klabu Bingwa Afrika
- Dirisha la usajili Tanzania 2024/2025 Kufungwa Leo Agosti 15
- Viingilio Mechi ya Vital O FC Vs Yanga Klabu Bingwa 17/08/2024
- Jezi Mpya Za Yanga 2024/2025
- Yanga Yapata Mserereko CAF: Mechi Zote za Klabu Bingwa Kupigwa Dar es Salaam
Weka Komenti