Wachezaji Wapya Azam 2024/2025 (Wachezaji Waliosajiliwa Azam FC)

Wachezaji Wapya Azam 2024/2025 (Wachezaji Waliosajiliwa Azam FC)

Klabu ya Azam FC imeanza rasmi kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2024/2025 kwa kuanza na kusajili wachezaji wapya ambao watavaa na kupambania jezi ya Azam katika michuano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025 na michuano ya Klabu Bingwa Afrika CAF. Msimu wa 2023/2024 ulikuwa ni msimu ambao Azam ilionesha kiwango kizuri ambapo waliweza kumaliza katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi mbele ya Simba SC ambao walimaliza katika nafasi ya tatu. Pia Azam waliweza kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB japo ndoto zao za kubeba ubingwa huo kuzimwa na Yanga SC kwa mikwaju ya penati.

Mataraji ya klabu ya Azam FC bila shaka yatakuwa ni kuendeleza ubabe walioonesha msimu uliopita huku juhudi za kufanya hivyo zimeanza kuonekana rasmi katika sajili zinazoendelea ambapo hadi sasa mabadiliko kadhaa yamefanyika kwa lengo la kuboresha kikosi cha Azam. Hapa tutakuletea orodha ya wachezaji wapya wa Azam FC 2024/2025.

Wachezaji Wapya Azam 2024/2025 (Wachezaji Waliosajiliwa Azam FC)

Dhamira ya Azam FC kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu wa 2024/2025 kwa kusajili wachezaji wapya wenye uwezo na uzoefu kutoka ndani na nje ya Tanzania imeanza kuonekana rasmi. Usajili huu unaashiria nia ya Azam FC kurejea kileleni mwa soka la Tanzania na kushindana vikali katika michuano ya kimataifa.

1. Yoro Mamadou Diaby

Wachezaji Wapya Azam 2024/2025-Yoro Mamadou Diaby

Diaby ni beki mwenye kipaji kutoka Mali ambaye ametokea katika akademi ya Yeleen Olympique, inayofahamika kwa kuzalisha vipaji vingi vya soka. Akiwa na umri wa miaka 23, Diaby ameiwakilisha Mali katika ngazi zote za timu za taifa za vijana na amekuwa nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya CHAN. Uwezo wake wa kuongoza safu ya ulinzi na kufunga mabao muhimu unatarajiwa kuimarisha Azam FC katika michuano yote.

2. Frank Tiesse

Frank Tiesse

Tiesse ni kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast ambaye amekuwa nahodha wa Stade Malien. Akiwa na umri wa miaka 26, Tiesse ameonyesha uwezo mkubwa wa kuchezesha timu, kutengeneza nafasi za mabao, na kufunga mabao muhimu. Uwezo wake wa kutembea na mpira na kutoa pasi za mwisho unatarajiwa kuwa nyongeza kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Azam FC.

3. Ever Meza

Ever Meza

Meza ni kiungo mwenye uwezo mkubwa kutoka Colombia ambaye anaweza kucheza nafasi zote za kiungo na hata beki wa kati. Akiwa na umri wa miaka 24, Meza ana uzoefu wa kucheza katika mashindano makubwa ya Copa Sudamericana. Uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi, kupiga pasi sahihi, na kuzuia mashambulizi ya wapinzani unatarajiwa kumfanya kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Azam FC.

4. Jhonier Blanco

Jhonier Blanco

Blanco ni mshambuliaji hatari kutoka Colombia ambaye alikuwa mfungaji bora wa ligi daraja la kwanza nchini humo msimu uliopita. Akiwa na umri wa miaka 24, Blanco anajulikana kwa uwezo wake wa kufunga mabao ya aina tofauti na kutafuta nafasi za kufunga. Uwepo wake unatarajiwa kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ya Azam FC na kuifanya kuwa tishio kwa wapinzani.

5. Nassor Saadun

Nassor Saadun

Azam imefanikiwa kumtangaza kiungo mshambuliaji, Nassor Saadun, kuwa mchezaji wao mpya kwa mkataba wa mwaka mmoja, wenye kipengele cha kuongeza mwengine. Nassor amejiunga na Azam akitokea klabu ya Geita Gold.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Azam Yatuma Ofa Kwa Simba Kumsajili Kipa Aishi Manula
  2. Tetesi za Usajili simba 2024/2025
  3. Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
  4. FIFA Yaiondolea Yanga Adhabu ya Kufungiwa Kusajili
  5. Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025
  6. Dirisha la Usajili Ligi Kuu Tanzania kufunguliwa Juni 15 hadi Agosti 15, 2024
  7. Wachezaji Walioachwa na Azam 2024/2025
  8. Azam Fc Yakubali Ombi La Prince Dube Kuvunja Mkataba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo