Orodha Ya Wafungaji Bora EPL Ligi Kuu Uingereza 2023/24 | Vinara Wa Magoli Ligi Kuu England EPL 2023/2024
Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2023/2024 umekuwa uwanja wa vita vya mabao, huku washambuliaji hatari wakipambana vikali kuwania Kiatu cha Dhahabu. Rekodi zimevunjwa, nyota wapya wamechipuka, na kila mechi imekuwa ni tamasha la kusisimua. Katika chapisho hili tunakuletea orodha kamili ya wafungaji bora EPL msimu huu, orodha ambayo itakuletea taarifa mpya na sahihi kila mara. Fuatilia kwa karibu ili kujua ni nani atakuwa mfalme wa mabao msimu huu wa kihistoria!
Orodha Ya Wafungaji Bora EPL Ligi Kuu Uingereza 2023/24
- Erling Haaland, Manchester City — Magoli 27
- Cole Palmer, Chelsea — Magoli 22
- Alexander Isak, Newcastle United — Magoli 20
- Ollie Watkins, Aston Villa — Magoli 19
- Dominic Solanke, Bournemouth — Magoli 19
- Mohamed Salah, Liverpool — Magoli 18
- Heung-min Son, Tottenham — Magoli 17
- Phil Foden, Manchester City — Magoli 17
- Jarrod Bowen, West Ham United — Magoli 16
- Bukayo Saka, Arsenal — Magoli 16
- Nicolas Jackson, Chelsea — Magoli 14
- Jean-Philippe Mateta, Crystal Palace — Magoli 13
- Leandro Trossard, Arsenal — Magoli 12
- Chris Wood, Nottingham Forest — Magoli 12
- Kai Havertz, Arsenal — Magoli 12
- Hee-chan Hwang, Wolverhampton Wanderers — Magoli 12
- Matheus Cunha, Wolves — Magoli 12
- Darwin Nunez, Liverpool — Magoli 11
- Richarlison, Tottenham Hotspur — Magoli 11
- Julian Alvarez, Manchester City — Magoli 11
- Yoane Wissa, Brentford — Magoli 11
- Anthony Gordon, Newcastle United — Magoli 10
- Leon Bailey, Aston Villa — Magoli 10
- Diogo Jota, Liverpool — Magoli 10
- Bruno Fernandes, Manchester United — Magoli 10
- Carlton Morris, Luton Town — Magoli 10
- Michael Olise, Crystal Palace — Magoli 10
- Elijah Adebayo, Luton Town — Magoli 10
- Douglas Luiz, Aston Villa — Magoli 9
- Rodrigo Muniz, Fulham — Magoli 9
- Callum Wilson, Newcastle United — Magoli 9
- Joao Pedro, Brighton — Magoli 9
- Eberechi Eze, Crystal Palace — Magoli 9
- Bryan Mbeumo, Brentford — Magoli 9
- Rasmus Hojlund, Manchester United — Magoli 9
- Martin Odegaard, Arsenal — Magoli 8
- Luis Diaz, Liverpool — Magoli 8
- Antoine Semenyo, Bournemouth — Magoli 8
Erling Haaland, mshambuliaji kutoka Norway ambae anaongoza safu ya ushambuliaji Manchester City, ameshika usukani kwa ubabe akiongoza orodha ya wafungaji akiwa na jumla ya magoli 27.
Huku akiwa tayari amevunja rekodi kadhaa msimu uliopita, Haaland anaendelea kuonyesha umahiri wake wa kufumania nyavu. Kasi yake, nguvu, na uwezo wake wa kukaa nafasi sahihi unamfanya kuwa tishio kwa mabeki wowote.
Japo kuwa nyota wa zamani wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, aliyetimkia Bayern Munich, ameacha pengo kubwa EPL. Hata hivyo, wachezaji wengine wamejitokeza kujaza nafasi yake. Cole Palmer wa Chelsea amekuwa moto wa kuotea mbali, akifunga mabao ya kila aina. Anthony Gordon na Alexander Isak wa Newcastle United wameunda ushirikiano hatari ulioipa timu yao mabao mengi.
Liverpool nao hawako nyuma, wakiongozwa na Mohamed Salah, Darwin Nunez, na Cody Gakpo. Utatu huu hatari umeifanya safu ya ushambuliaji ya Liverpool kuwa moja ya zinazo ogopwa zaidi Ulaya. Arsenal nao wamepata nguvu mpya kupitia Leandro Trossard na Bukayo Saka, ambao wamekuwa wakifunga mabao muhimu.
Katika kinyang’anyiro hiki cha Kiatu cha Dhahabu, kila bao lina thamani kubwa. Huku msimu ukielekea ukingoni, mashabiki wa soka duniani kote wanasubiri kwa hamu kuona ni nani atakayebeba tuzo hii ya kifahari. Je, Haaland ataendeleza ubabe wake? Au Labda mmoja wa nyota chipukizi atashangaza ulimwengu wa soka?
Bila shaka, msimu wa 2023/2024 utaingia katika vitabu vya historia vya EPL kama mmoja wa misimu iliyokuwa na ushindani mkubwa katika kuwania Kiatu cha Dhahabu. Wafungaji bora wa msimu huu watakuwa wameacha alama isiyofutika katika historia ya soka England.
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti