Yanga Yafukuzisha Kocha Mamelodi Sundowns

Yanga Yafukuzisha Kocha Mamelodi Sundowns – Sababu na Maelezo Kamili

Mabingwa wa soka Afrika kusini Mamelodi Sundowns wameamua kusitisha mkataba wa kocha wao, Rulani Mokwena, kufuatia matokeo yasiyoridhisha ya msimu uliopita. Timu hiyo ya Afrika Kusini ilishindwa kung’ara katika mashindano muhimu, ikiwa ni pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions league), ambapo licha ya kuiondo Yanga Sc katika hatua ya robo fainali kwa mikwaju ya penati, Sundowns ilionesha kiwango ambacho hakukuridhisha mashabiki wengi wa timu hiyo pamoja na viongozi wa juu.

Hata ivo, ndoto za Sundowns za kufika hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrka zilizimwa na mabingwa wa soka kutoka Tunisia baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya mabingwa wa Afrika.

Yanga Yafukuzisha Kocha Mamelodi Sundowns

Sababu za Kuondolewa kwa Mokwena

Matokeo mabaya ya Mamelodi Sundowns msimu uliopita ni moja ya sababu kuu za uamuzi huu. Timu hiyo ilikutana na Yanga SC mara mbili, ambapo mechi ya kwanza ilifanyika Machi 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa sare ya bila mabao. Mechi ya marudiano ilichezwa Aprili 5 nchini Afrika Kusini na pia kumalizika bila bao, huku Mamelodi ikisonga mbele kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2, baada ya Yanga kukataliwa bao lililofungwa na Stephen Aziz Ki.

Uongozi wa Mamelodi Sundowns ulifanya kikao cha tathmini na Mokwena mwanzoni mwa wiki hii, ambapo walijadili mafanikio na changamoto za msimu uliomalizika. Baada ya tathmini hiyo, waliamua kusitisha mkataba wa kocha huyo kwa sababu ya kushindwa kufikia malengo waliyokuwa wamejiwekea.

Moja ya viongozi wa Mamelodi alieleza, “Ameshindwa kufikia malengo. Ndiyo sababu inayotusukuma kuachana naye. Atatangazwa muda wake ukifika.”

Malengo Aliyoshindwa Kufikia

Mokwena, ambaye alikuwa visiwani Zanzibar kwa mapumziko wiki mbili zilizopita, alishindwa kufikisha timu yake kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na pia alipoteza ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Nchi hiyo (Nedbank Cup) kwa kufungwa 2-1 na Orlando Pirates. Mafanikio pekee aliyopata msimu uliopita ni kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Afrika Kusini.

Wachezaji Walioachwa na Mamelodi Sundowns

Mbali na kumfuta kazi kocha Mokwena, Mamelodi Sundowns pia imetangaza kuachana na wachezaji wake wanne. Wachezaji hao ni Bongani Zungu, Brian Onyango, Gaston Sirino, na Thabiso Kutumela. Hii ni sehemu ya mabadiliko makubwa yanayofanywa na klabu hiyo ili kurejesha hadhi na nguvu yake katika mashindano mbalimbali.

Hitimisho

Hatua ya Mamelodi Sundowns kuachana na kocha Rulani Mokwena ni ishara ya kujitathmini na kutafuta mwelekeo mpya baada ya msimu wa kuvunja moyo. Matokeo mabaya dhidi ya Yanga SC yamechangia kwa kiasi kikubwa uamuzi huu, na sasa Mamelodi inajiandaa kwa mabadiliko makubwa katika benchi la ufundi na kikosi chake ili kurejea kwenye nafasi ya juu katika soka la Afrika.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Jean Charles Ahoua Kurithi Mikoba ya Chama Simba 2024/2025
  2. Cv Ya Steven Mukwala Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025
  3. Orodha ya Mabingwa wa Kombe La Shirikisho Tanzania
  4. Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo