Yanga Yatangaza Kumsajili Duke Abuya: Klabu ya Yanga imezidi kuimarisha kikosi chake kwa kutambulisha kiungo wa boli Duke Abuya kuelekea msimu wa 2024/2025. Hii ni hatua muhimu kwa klabu ambayo imekuwa ikijiandaa kwa muda mrefu kuhakikisha inakuwa na kikosi imara kinachoweza kushindana katika michuano yote, ndani na nje ya nchi. Hatua hii ya kumsajili Abuya inakuja baada ya uvumi uliodumu kwa wiki kadhaa kuhusu uhamisho wake.
Yanga Yatangaza Kumsajili Duke Abuya
Duke Abuya, ambaye ametambulishwa rasmi na timu ya wananchi akitokea Sigida Black Stars (Ihefu SC), ni mchezaji mwenye uwezo wa kipekee wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani. Anajulikana kwa uwezo wake wa kucheza kama kiungo mkabaji, kiungo mshambuliaji, na hata winga wa kulia. Uwezo wake wa kucheza katika nafasi hizi tofauti unampa kocha wa Yanga Miguel Ángel Gamondi chaguo zaidi katika kupanga kikosi, hasa wakati wa mechi muhimu.
Abuya anakua mchezaji wa sita kuongezwa katika kikosi cha Yanga kuelekea msimu wa 2024/2025. Wachezaji wengine ambao wameshatambulishwa na klabu ni pamoja na Clatous Chama, Prince Dube, Boka Chadrak, Khomeini Abubakar na Aziz Andabwile
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti