Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba | Historia ya Joshua Mutale Timu Alizochezea: Joshua Mutale ni mmoja kati ya wachezaji mahiri ambao wametambulishwa kujiunga na klabu ya Simba Sc ambayo kwa sasa ipo katika uboreshaji wa kikosi chake kuelekea msimu wa 2024/2025. Mutare ni mchezaji wa pili kutambulishwa baada ya Lawi ambae alitambulishwa tarehe 20 juni 2024.
Joshua Mutale ana umri wa miaka 22 na ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani kwa ufanisi wa hali ya juu, Joshua anaweza kumudu nafasi ya winga ya kulia, kushoto, na wakati mwingine anacheza nyuma ya mshambuliaji, yaani namba 10. Akiwa na timu ya Power Dynamos msimu uliopita, Mutale alifanikiwa kufunga mabao matano na kuisaidia timu yake kupata mengine matatu katika michezo 26.
Uwezo wake wa kumudu kucheza nafasi nyingi uwanjani pamoja na umri wake mdogo, ni miongoni mwa vigezo vilivyovutia klabu ya Simba kumsajili. Huu ni mkakati maalumu wa klabu ya Simba wa kuboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji vijana wenye ubora. Mutale anatarajiwa kuleta mchango mkubwa katika timu kwa msimu ujao na kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Simba.
Katika makala hii, tutachambua kwa undani maisha yake ya soka, kuanzia mwanzo wake hadi alipo sasa akiwa mchezaji wa Simba SC. Tutazungumzia historia yake, ufanisi wake katika klabu, mchango wake katika timu ya taifa, mtindo wake wa uchezaji, na tuzo alizoshinda. Pia, tutaangazia maisha yake binafsi na matarajio yake ya baadaye katika ulimwengu wa soka.
Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji Mpya wa Simba 2024/2025
- Tarehe ya kuzaliwa: Januari 24, 2002
- Mahali pa kuzaliwa: Zambia
- Umri: 22
- Urefu: 1.65 m
- Uraia: Zambia
- Nafasi: Winga wa Kulia
- Klabu ya zamani: Power Dynamos FC
- Klabu ya sasa: Simba SC
- Nafasi kuu Anayocheza: Winga wa Kulia
- Nafasi nyingine: Winga wa Kushoto na Mshambuliaji wa Pili
Mapendekezo Ya mhariri:
- Azam Yatuma Ofa Kwa Simba Kumsajili Kipa Aishi Manula
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Wachezaji Wapya Simba 2024/2025
- Simba Day 2024: Tarehe Rasmi Yatangazwa na Simba SC
- Mishahara Ya Wachezaji Wa Simba 2024/2025
- Wachezaji walioachwa na Simba 2024/2025
- Kikosi Cha Simba 2024/2025 | Wachezaji Wote wa Simba
- Wachezaji Walio Ongeza Mkataba Simba 2024/2025
Weka Komenti