England vs Hispania: Matokeo ya Fainali ya EURO 2024

England vs Hispania: Matokeo ya Fainali ya EURO 2024

Usiku wa kusisimua unakaribia katika Uwanja wa Olympiastadion, Berlin, ambapo miamba wa soka Ulaya, England na Hispania, watapambana vikali kuwania taji la mabingwa wa bara la Ulaya ijulikanayo kama EURO 2024. Mtanange huu wa fainali una historia ndefu na takwimu za kusisimua, na mashabiki wa soka kote duniani wanajiuliza. Fainali hii inaweza kua ni fursa ya Hispania kujinyakulia taji lao la nne la Ulaya, wakati Uingereza inatafuta kumaliza ukame wa miaka 58 bila taji la kimataifa. Je, ni Simba wa Uingereza watakaonguruma, ama La Roja ya Hispania watawika tena?

Safari ya England na Hispania Kuelekea Fainali ya EURO 2024

Timu zote mbili zimeonyesha kiwango cha hali juu hadi kufika fainali hii ambayo inatarajiwa kuchezeka leo hii julai 14 2024 saa nne usiku.

Hispania, wakiwa mabingwa mara tatu wa Ulaya, wamekuwa moto wa kuotea mbali, wakithibitisha ubora wa kikosi chao kilicho jaa nyota chipukizi kwa kuwatoa vigogo kama Ujerumani na Ufaransa. Lamine Yamal, kinda mwenye umri wa miaka 17 tu, amekuwa nyota angavu katika kikosi cha La Roja, akifunga na kutoa pasi za mabao kwa ustadi mkubwa.

England, kwa upande wao, wamepitia njia yenye misukosuko, wakilazimika kupambana hadi dakika za mwisho katika mechi kadhaa. Hata hivyo, ushupavu wao na ari ya kupigania ushindi umewapa tiketi ya fainali hii ya kihistoria. Harry Kane, kinara wa mabao wa Uingereza, atakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha Simba wa Uingereza wanang’oa taji lao la kwanza la Ulaya tangu mwaka 1966.

Matokeo ya Fainali ya EURO 2024 England vs Hispania

England 1-2Hispania
  • Wafungaji Magoli Hispania; Nico Williams – 47’Mikel Oyarzabal – 86′
  • Mfungajio wa Goli la England; Cole Palmer – 73′

England vs Hispania: Matokeo ya Fainali ya EURO 2024

Historia ya England vs Hispania Michezo Iliyopita

Katika historia, England na Hispania wamekutana mara 27 katika mechi rasmi, na Uingereza wakiwa na ushindi mara 14, sare tatu, na Hispania mara 10. Hata hivyo, takwimu hizi hazitoi picha kamili. Mechi za hivi karibuni zimekuwa ngumu, na ushindi ukitawaliwa na timu moja au nyingine. Mtanange huu wa fainali, bila shaka, utakuwa na sura yake ya kipekee.

Idadi ya Michezo Waliokutana27
Mechi Alizoshinda Hispania10
Sare3
Mechi Alizoshinda England14

Matokeo ya Mechi kati ya Uingereza na Hispania

TareheMatokeoMashindano
Oktoba 15, 2018Hispania 2-3 UingerezaLigi ya Mataifa, Awamu ya Ligi
Septemba 08, 2018Uingereza 1-2 HispaniaLigi ya Mataifa, Awamu ya Ligi
Novemba 15, 2016Uingereza 2-2 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Novemba 13, 2015Hispania 2-0 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Novemba 12, 2011Uingereza 1-0 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Februari 11, 2009Hispania 2-0 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Februari 7, 2007Uingereza 0-1 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Novemba 17, 2004Hispania 1-0 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Februari 28, 2001Uingereza 3-0 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Juni 22, 1996Uingereza 0-0 Hispania (penalti 4-2)Mashindano ya Ulaya, Robo-Fainali
Septemba 9, 1992Hispania 1-0 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Februari 18, 1987Hispania 2-4 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Julai 5, 1982Hispania 0-0 UingerezaKombe la Dunia, Awamu ya Makundi
Machi 25, 1981Uingereza 1-2 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Juni 18, 1980Uingereza 2-1 HispaniaMashindano ya Ulaya, Awamu ya Makundi
Machi 26, 1980Hispania 0-2 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Mei 8, 1968Hispania 1-2 UingerezaMashindano ya Ulaya, Robo-Fainali ya Mchujo
Aprili 3, 1968Uingereza 1-0 HispaniaMashindano ya Ulaya, Robo-Fainali ya Mchujo
Mei 24, 1967Uingereza 2-0 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Desemba 8, 1965Hispania 0-2 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Oktoba 26, 1960Uingereza 4-2 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Novemba 30, 1955Uingereza 4-1 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Mei 18, 1955Hispania 1-1 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Julai 02, 1950Hispania 1-0 UingerezaKombe la Dunia la FIFA
Desemba 09, 1931Uingereza 7-1 HispaniaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Mei 15, 1929Hispania 4-3 UingerezaMechi ya Kirafiki ya Kimataifa

Uchambuzi: Mbinu na Wachezaji Muhimu

Spain wanatarajiwa kuja na mbinu yao ya tiki-taka, wakipiga pasi nyingi na kutawala mpira kwa muda mrefu. Wachezaji wao mahiri, kama vile Pedri, Gavi, na Dani Olmo, watajaribu kuvuruga safu ya ulinzi ya Uingereza. Kwa upande wao, England watategemea kasi ya wachezaji kama Bukayo Saka na Raheem Sterling kushambulia kwa kushtukiza huku uzoefu na uwezo wa nyota wa england kama Harry Kane unatarajiwa kua msaada mkubwa.Pia Jude Bellingham, atakuwa na jukumu la kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Timu Zilizofuzu Robo Fainali EURO 2024 & Ratiba
  2. Msimamo Makundi ya EURO 2024
  3. Matokeo Ya Mechi Za Euro 2024
  4. Ratiba Kamili ya UEFA Euro 2024 Hatua Ya 16 Bora
  5. Timu zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Euro 2024
  6. Wafungaji Bora EURO 2024: Hawa Ndio Vinara Wa Magoli
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo