Chama Kuvaa Jezi Namba 17 Yanga Msimu Ujao
Katika msimu ujao wa ligi kuu ya NBC Tanzania, Klabu ya Yanga SC imethibitisha kuwa kiungo wao mpya, Clatous Chama, atavaa jezi namba 17 ambayo apo awali kabla ya usajili wa Chama ilikua ikivaliwa na Farid Musa. Uhamisho huu unakuja baada ya Chama kujiunga na Yanga akitokea Simba SC kama mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na klabu hiyo.
Habari za ndani kutoka kambi ya mazoezi ya Yanga, iliyopo Avic Town, Kigamboni, Dar es salaam zinafichua kwamba Chama aliomba kuvaa jezi namba 17, lakini alikuta tayari jezi hiyo imeshachukuliwa na Farid Mussa, kiungo mwenzake ambae aliongeza mkataba wake na Yanga hadi 2026. Farid alikubali kumwachia Chama jezi hiyo muhimu, huku yeye akichagua kuvalia namba 28.
Uamuzi huu wa Farid unadhihirisha umoja na mshikamano uliopo ndani ya kikosi cha Yanga. Chama, kwa upande wake, amekuwa akiipenda sana jezi namba 17, ambayo ameizoea tangu akiwa na timu ya taifa ya Zambia na Simba kwa miaka sita iliyopita.
Mabadiliko ya jezi hayakuwa kwa Chama pekee. Jonas Mkude, kiungo mwingine aliyejiunga na Yanga msimu uliopita kutoka Simba, naye atapata fursa ya kuvaa jezi yake ya bahati, namba 20. Msimu uliopita, Mkude alilazimika kuvaa namba 19 kwa sababu namba 20 ilikuwa inamilikiwa na Zawadi Mauya. Lakini kwa sasa, baada ya Mauya kuondoka Yanga, Mkude amechukua nafasi hiyo kuvaa jezi ambayo amekuwa akiitumia kwa zaidi ya miaka 10 akiwa Simba na timu ya taifa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Djigui Diarra Warejea Mazoezini
- Cv ya Karaboue Chamou Beki Mpya Wa Simba 2024/2025
- Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba
- Jemedari Said Kazumari Atangazwa kua CEO Mpya JKT Tanzania
- Inonga Baka Atambulishwa Klabu ya AS FAR Rabat Morocco
- Hispania Yaibuka Mabingwa wa EURO 2024 Baada ya Kuichapa Uingereza 2-1
- Kocha Mpya Wa JKT Tanzania 2024/2025
- England vs Hispania: Matokeo ya Fainali ya EURO 2024
- Ratiba Ya Simba Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup 2024/2025
- Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2024/2025 Hatua ya Awali
- Ifahamu Timu ya Vital’O Mpinzani wa Yanga CAF Champions league
- Yanga Yatangaza Kumsajili Duke Abuya
Weka Komenti