Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025 | Wachezaji walioitwa Taifa star 2024 | Kikosi cha Taifa Stars 2024/2025
Kikosi cha Taifa Stars, chini ya Kaimu Kocha Mkuu Hemed Suleiman, kimetajwa rasmi kuanza maandalizi kwa ajili ya michezo miwili muhimu ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Maandalizi haya ni sehemu muhimu ya mkakati wa timu ya Taifa Stars kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Kocha Hemed Suleiman ameteua wachezaji 23 ambao wataingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Ethiopia na Guinea. Michezo hiyo itachezwa tarehe 4 Septemba na 10 Septemba 2024, ikiwa na umuhimu mkubwa katika safari ya kufuzu katika michuano ya AFCON 2025 ambayo inatarajiwa kufanyika Morocco.
Kikosi hiki kimejumuisha wachezaji wenye vipaji na uzoefu kutoka klabu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Wachezaji wa Yanga SC na Simba SC wakiwa na wawakilishi wengi, huku pia kukiwa na wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania kama Himid Mao anayekipiga Tala’a El Geish ya Misri na Cyprian Kachwele anayechezea Vancouver Whitecaps nchini Canada.
Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025
Orodha ya wachezaji walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
- Ally Salim – Simba SC
- Abdultwalib Mshery – Young Africans
- Yona Amos – Pamba SC
- Lusajo Mwaikenda – Azam FC
- Nathaniel Chilambo – Azam FC
- Mohamed Hussein – Simba SC
- Dickson Job – Young Africans
- Pascal Msindo – Azam FC
- Ibrahim Hamad – Young Africans
- Bakari Nondo – Young Africans
- Nickson Kibabage – Young Africans
- Abdulmalik Zakaria – Mashujaa FC
- Adolf Mtasigwa – Azam FC
- Himid Mao – Tala’a El Geish, Misri
- Novatus Dismas – Goztepe, Uturuki
- Mudathir Yahya – Young Africans
- Hussein Semfuko – Coastal Union
- Edwin Balua – Simba SC
- Feisal Salim – Azam FC
- Wazir Junior – Dodoma Jiji
- Cyprian Kachwele – Vancouver Whitecaps, Canada
- Clement Mzize – Young Africans
- Abel Josiah – TDS TFF Academy
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025
- Tabora united Yaibuka na Ushindi wa 2-1 Dhidi ya Namungo
- Ratiba Ya Simba Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup 2024/2025
- Ifahamu CBE SA Ya Ethiopia Wapinzani wa Yanga Klabu Bingwa
- Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
- Pesa Iliyochukua Yanga Goli la Mama Klabu Bingwa 2024
- Yanga Kucheza na CBE SA Ya Ethiopia Klabu Bingwa Septemba 2024
Weka Komenti