Kipa wa CBE Aeleza Hofu Yake Kuelekea Mchezo wa Pili Ligi ya Mabingwa
MASHABIKI wa Yanga bado wanasubiri kuona mabadiliko ya washambuliaji wao kuelekea mechi ya mkondo wa pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini kipa wa wapinzani wao hao bado anawawaza washambuliaji wa timu hiyo akimtaja Prince Dube.
Kipa Firew Alemayehu wa CBE ameliambia Mwanaspoti kuwa bado haamini kama wapinzani wao walishinda kwa bao 1-0 pekee kutokana na mashambulizi mengi waliyowasukumia akisema bado wana safari ngumu kuwang’oa Mabingwa hao wa Tanzania
Alemayehu alisema Yanga imewapa kazi ngumu kuona ndoto yao ya kwenda kushiriki hatua ya makundi kwa mara ya kwanza ni ngumu kwani washambuliaji wao watabadilika tu kuelekea mchezo wa marudiano.
Kipa huyo alisema kuwa Dube licha ya kupoteza nafasi nyingi za kufunga akifunga bao Moja pekee bado ni mshambuliaji wanapotakiwa kumchunga kuelekea mchezo huo wa marudiano utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Septemba 21 mwaka huu.
“Bado tuna mchezo mgumu dhidi ya Yanga, unajua ukiangalia mechi iliyopita unaona kwamba ni kama walikosa bahati tu au sisi tulikuwa na bahati ni timu Bora,” alisema Alemayehu ambaye ni kipa namba mbili wa Taifa lake la Ethiopia.
“Hata yule aliyetufunga (Dube) nadhani ni kama alikuwa hana siku nzuri mchezoni lakini ukitazama anavyojua kujiweka mazingira mazuri utagundua bado ni mchezaji hatari.
“Tunatakiwa kujiandaa sawasawa vinginevyo mchezo wetu wa marudiano utakuwa mgumu zaidi kwani watakuja na presha kubwa ya kujisahihisha makosa yao.”
Mapendekezo ya Mhariri:
- Marefa Mechi za Simba na Yanga Klabu Bingwa Afrika
- Viingilio Mechi ya Yanga Vs CBE 21/09/2024
- Vituo Vya Kukata Tiketi Mechi ya Yanga Vs CBE 21/09/2024
- Mbappe Aanza na Goli Mechi ya Kwanza UEFA Akiwa na Madrid
- Fei Toto Atamani Bato Lake na Aziz Ki liendelee
- Kenya, Uganda na Tanzania Kuandaa CHAN 2024 – Fainali Kuanza Februari
Weka Komenti