Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON 2025 | Taifa Stars Yapangwa Kundi H kufuzu AFCON 2025
Droo ya hatua ya makundi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 imefanyika nchini Afrika Kusini, na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imejipata ikipangwa katika kundi moja lenye vigogo wa soka Afrika. Kundi hili ambalo mashabiki wa soka Tanzania wamelipa jina la utani “Kundi la Kifo.” Je, Tanzania Taifa stars itathibitisha ubora wake na kupata tiketi ya safari ya kuelekea Morocco? Ni swala la muda tu kabla mbivu na mbichi kujulikana kuelekea katika michuano hii ya kitaifa Afrika.
Kundi H Ndio Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON 2025
Taifa Star imepangwa Kundi H, ikiwa timu ya pili baada ya Ethiopia, huku Guinea na DR Congo zikifuata. Kwa mujibu wa viwango vya ubora vya FIFA vilivyotolewa Juni 2023, DR Congo inaongoza katika kundi hilo ikiwa nafasi ya 61, ikifuatiwa na Guinea (77), Tanzania (114), na Ethiopia (143). Uwepo wa Tanzania na DR Congo katika kundi kumerejesha kumbukumbu za mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2022 ambapo timu hizi zilikutana katika makundi na kutoa matokeo ya sare ya 1-1 ugenini kwa Tanzania na kufungwa 3-0 nyumbani. Katika mashindano ya AFCON 2023, timu hizi zilikutana tena na kutoa sare ya 0-0.
Timu Za Kundi H Kufuzu AFCON 2025 2025
- Ethiopia
- Tanzania
- Guinea
- DR Congo
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti