Khomeini Abubakar Ajiunga na Yanga Akitokea Singida Black Star: Klabu ya Yanga SC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la shirikisho la CRDB bank, wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa kumsajili mlinda mlango chipukizi Aboubakar Khomeini kutoka Singida Black Stars. Usajili huu unaonesha nia ya dhati ya Yanga kuendeleza utawala wao katika soka la Tanzania.
Rasmi: Khomeini Abubakar Ajiunga na Yanga Akitokea Singida Black Star
Khomeini, ambaye awali alijipatia umaarufu akiwa na Ihefu SC, amekuwa gumzo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchomoa mashuti. Kipa huyu mwenye umri mdogo pia ameonyesha kiwango cha hali ya juu akiwa anaichezea klabu ya Singida Black Stars, na sasa anajiunga na mabingwa wa ligi kuu ya NBC Tanzania (Yanga sc) akiwa tayari kuchukua majukumu makubwa zaidi.
Uwezo wake wa kuokoa michomo ya hatari, kuongoza safu ya ulinzi, na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma umemfanya kuwa mmoja wa makipa wanaochipukia kwa kasi zaidi nchini. Usajili wake unatarajiwa kuongeza ushindani wa hali ya juu katika nafasi ya mlinda mlango ndani ya Yanga.
Usajili wa Khomeini unakuja baada ya Yanga kuwanasa wachezaji wengine watatu wenye uwezo mkubwa. Wachezaji wengine ambao wameshatangazwa na klabu ya Yanga ni pamoja na;
- Chadrack Issaka Boka: Beki wa kushoto mwenye kasi na uwezo wa kushambulia kutoka St Eloi Lupopo ya DRC.
- Clatous Chota Chama: Kiungo mshambuliaji mwenye uzoefu na uwezo wa kufunga mabao kutoka Simba SC.
- Prince Dube Mpumelelo: Mshambuliaji hatari mwenye uwezo wa kufunga mabao ya kila aina kutoka Azam FC.
Kwa kuongeza nyota hawa wapya kwenye kikosi chao kilichopo, Yanga inaonyesha dhamira ya kuendelea kutawala soka la Tanzania na kufanya vyema katika michuano ya kimataifa.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti