Mashujaa Fc Imetangaza Kumsajili Carlos Protus
Klabu ya soka ya Mashujaa FC imetangaza rasmi kumsajili mlinzi mahiri, Carlos Protus, kwa ajili ya msimu ujao wa 2024/2025. Hii ni hatua kubwa kwa klabu hiyo ambayo inajiandaa kukabiliana na timu zenye uzoefu mkubwa ligi kuu ukizingatia wenyewe ndo wanashiriki kwa mara ya pili. Usajili huu unaleta matumaini mapya kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na kiwango cha Carlos Protus.
Carlos Protus, ambaye amesaini mkataba wa kuichezea Mashujaa FC kwa msimu mzima, amejipatia umaarufu kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kucheza kama beki. Alikuwa mchezaji wa klabu ya Biashara United Mara, ambayo inashiriki Ligi ya Championship. Protus amejijengea jina kutokana na uwezo wake wa kujilinda vizuri, kusoma mchezo, na kutoa msaada mkubwa kwa safu ya ulinzi ya timu.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti