Mwisho Wa Kutuma Maombi ya Vyuo Vya Diploma NACTVET | Tarehe za Mwisho Udahili Kwa 2024/2025 Ngazi ya Astashahada na Stashahada NACTE
Kama wewe ni muhitimu wa Kidato cha Nne au Kidato cha Sita mwenye malengo ya kujiunga na elimu ya juu ngazi ya Astashahada na Stashahada katika kozi zote zinazosimamiwa na NACTVET basi huu ndio wakati sahihi wa kutuma maombi katika chuo unachotamani kujiunga nacho. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limefungua rasmi udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2024/2025 na fursa hii inakaribia kufungwa.
National Council for Technical and Vocational Education and Training (NACTVET) inatoa fani mbalimbali ikiwemo uhandisi, teknolojia, kilimo na biashara. Elimu ya ufundi stadi itakayokupa ujuzi wa vitendo unaohitajika sana katika soko la ajira la sasa. Hii ni fursa ya kipekee ya kutimiza ndoto zako na kujipatia ujuzi utakaokuwezesha kuajiriwa au kujiajiri. Usisubiri hadi dakika ya mwisho, chukua hatua sasa na utume maombi yako leo! Fursa hii ya kipekee ya kubadilisha maisha yako inakusubiri, usikose!
Kuhusu Vyuo Vya Diploma Vya NACTVET
Vyuo vinavyosimamiwa na NACTVET vinatoa elimu bora na ya kisasa katika fani mbalimbali za ufundi stadi. Hii inakupa wewe mhitimu ujuzi unaohitajika sana katika soko la ajira la sasa. Baadhi ya faida za kujiunga na vyuo hivi ni pamoja na:
- Ujuzi wa Vitendo: Elimu ya ufundi stadi inakupa ujuzi wa vitendo unaokutayarisha vyema kwa ajira au kujiajiri.
- Fani Mbalimbali: NACTVET inasimamia vyuo vinavyotoa mafunzo katika fani mbalimbali kama vile uhandisi, teknolojia, kilimo, biashara, na nyingine nyingi.
- Ajira na Kujiajiri: Wahitimu wa vyuo vya NACTVET wana uwezo mkubwa wa kupata ajira au kujiajiri na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Mwisho Wa Kutuma Maombi ya Vyuo Vya Diploma NACTVET
- Mwisho wa Maombi: Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi kwa kozi zisizohusiana na afya na sayansi shirikishi, pamoja na kozi zinazotolewa Zanzibar, ni tarehe 14 Julai, 2024.
- Mwisho wa Maombi ya CAS: Kwa kozi za afya na sayansi shirikishi zinazotolewa Tanzania Bara, maombi yatafanyika kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) hadi tarehe 30 Juni, 2024.
Jinsi ya Kutuma Maombi
- Kozi zisizohusiana na afya na sayansi shirikishi na kozi zinazotolewa Zanzibar: Maombi yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.
- Kozi za afya na sayansi shirikishi Tanzania Bara: Maombi yatumwe kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaopatikana kwenye tovuti ya NACTVET (www.nactvet.go.tz).
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti