Thamani ya Kombe la Club Bingwa Afrika 2024/2025 | Thamani ya Kombe la Klabu Bingwa CAF Champions league 2024
Katika msimu wa 2024/2025 wa michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika, Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limechukua hatua kubwa katika kuboresha thamani ya mashindano haya kwa kutoa motisha ya kifedha kwa klabu zinazoshiriki. Rais wa CAF, Dr. Patrice Motsepe, aliahidi kuimarisha mashindano ya vilabu barani Afrika na kutoa msaada wa kifedha kwa klabu zinazoshiriki, jambo ambalo sasa limetimia kupitia ongezeko kubwa la zawadi za fedha kwa washindi na pia msaada kwa klabu zinazoshiriki hatua za awali za michuano.
Zawadi za Fedha kwa Hatua za Awali
Kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya CAF, vilabu vinavyoshiriki hatua za awali (Preliminary Round) za michuano ya TotalEnergies CAF Champions League na TotalEnergies CAF Confederation Cup vitapokea dola 50,000 kila moja kama msaada wa kifedha. Hapo awali, vilabu vililazimika kufika hatua ya makundi ili kuweza kushiriki kwenye mgao wa zawadi za fedha.
Hatua hii inalenga kusaidia vilabu kukabiliana na gharama za usafiri na mipango ya kiufundi ambayo imekuwa ikiwakabili klabu nyingi za Afrika zinazoshiriki mashindano ya kimataifa.
Thamani ya Kombe la Club Bingwa Afrika 2024/2025
CAF imeongeza kiasi cha fedha kwa washindi wa michuano ya TotalEnergies CAF Champions League na TotalEnergies CAF Confederation Cup. Washindi wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) sasa watapata dola za Kimarekani milioni 4, ikilinganishwa na dola milioni 2.5 walizopokea mwaka 2022. Hii ni ongezeko la asilimia kubwa ambalo linalenga kuongeza ushindani na thamani ya taji hili kuu barani Afrika.
Kwa upande wa Kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup), mshindi sasa atazawadiwa dola milioni 2, tofauti na dola milioni 1.2 zilizokuwa zikitolewa mwaka 2022. Ongezeko hili linaonyesha dhamira ya CAF katika kuboresha hali ya kifedha ya vilabu vinavyoshiriki michuano hii. CAF imeandaa muundo mpya wa zawadi za fedha kwa michuano hii kwa mwaka 2024/2025 kama ifuatavyo:
- Mshindi: Dola za Kimarekani milioni 4
- Mshindi wa pili: Dola za Kimarekani milioni 2
- Nusu fainali: Dola za Kimarekani milioni 1.2
- Robo fainali: Dola za Kimarekani 900,000
- Nafasi ya tatu katika kundi: Dola za Kimarekani 700,000
- Nafasi ya nne katika kundi: Dola za Kimarekani 700,000
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti