Viingilio Mechi ya Simba Vs Coastal Union 04/10/2024
Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanasubiri kwa hamu kubwa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba SC na Coastal Union, itakayochezwa tarehe 4 Oktoba 2024 katika uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Mchezo huu ni miongoni mwa michezo inayotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki kutokana na rekodi nzuri ya Simba SC mwanzoni mwa msimu huu wa 2024/2025.
Simba SC, maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, wameonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu, wakishinda mechi zote nne walizocheza na kufunga mabao 10 bila kuruhusu goli hata moja. Timu hiyo kwa sasa inashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi Tanzania bara, wakiwa na jumla ya pointi 12. Kwa mashabiki wa Simba wanaotaka kushuhudia timu yao ikiendeleza rekodi hiyo nzuri uwanjani, ni muhimu kufahamu viingilio vya mechi hii ili kujiandaa mapema. Viingilio vimepangwa kwa namna tofauti ili kuendana na mahitaji na uwezo wa mashabiki wa Simba SC na Coastal Union.
Viingilio Mechi ya Simba Vs Coastal Union 04/10/2024
Viingilio vya mechi ya Simba dhid ya Coastal Union ni kama ifuatavyo:
- VIP A: Tsh 20,000
- Mzunguko: Tsh 10,000
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ahoua Aingilia Kati Vita ya Assist Ligi Kuu, Awaburuza Feitoto na Aziz Ki
- Yanga Yaanza Mkakati wa Kurejea Kileleni mwa Msimamo wa Ligi kuu
- Ratiba ya Taifa Stars vs DR Congo Kufuzu AFCON 2025
- Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Dhidi ya DR Congo Kufuzu AFCON 2025
- Dodoma Jiji Fc vs Tabora United Leo 02/10/2024 Saa Ngapi?
- Acheni Kulewa Sifa – Kocha Coastal Union Awachana Chipukizi
Weka Komenti