Wachezaji Walioitwa Timu ya Taifa Kufuzu Afcon 2025 | Wachezaji Walioitwa Taifa Stars 2024 Michuano Kufuzu AFCON
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka wazi majina ya wachezaji watakaojiunga na kambi ya maandalizi ya Timu ya Taifa Stars kwa ajili ya michezo miwili muhimu ya kufuzu kwa michuano ya Afrika Cup of Nations (AFCON) 2025. Timu ya Taifa Stars inatarajiwa kucheza dhidi ya Ethiopia na Guinea katika juhudi za kupata nafasi ya kushiriki kwenye fainali za AFCON 2025.
Kocha Hemed Suleiman ameita kikosi kinachojumuisha wachezaji wanaofanya vizuri kutoka vilabu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi. Wachezaji hao wamechaguliwa kwa umakini mkubwa kulingano na uwezo wao wa kulisakata kabumbu ili kuhakikisha kuwa Taifa Stars inakuwa na kikosi imara na kinachoweza kukabiliana na ushindani mkali wa kimataifa.
Kambi ya maandalizi inatarajiwa kufanyika nchini Misri, ambapo wachezaji watajinoa vilivyo kabla ya kuanza kwa michezo hiyo miwili ya kufuzu. Huu ni mwanzo wa safari ya timu ya Taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars kuonyesha uwezo wao na kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki kwenye fainali za AFCON 2025.
Wachezaji Walioitwa Timu ya Taifa Kufuzu Afcon 2025
- Ally Salim – Simba SC
- Abdultwalib Mshery – Young Africans
- Yona Amos – Pamba SC
- Lusajo Mwaikenda – Azam FC
- Nathaniel Chilambo – Azam FC
- Mohamed Hussein – Simba SC
- Dickson Job – Young Africans
- Pascal Msindo – Azam FC
- Ibrahim Hamad – Young Africans
- Bakari Nondo – Young Africans
- Nickson Kibabage – Young Africans
- Abdulmalik Zakaria – Mashujaa FC
- Adolf Mtasigwa – Azam FC
- Himid Mao – Tala’a El Geish, Misri
- Novatus Dismas – Goztepe, Uturuki
- Mudathir Yahya – Young Africans
- Hussein Semfuko – Coastal Union
- Edwin Balua – Simba SC
- Feisal Salim – Azam FC
- Wazir Junior – Dodoma Jiji
- Cyprian Kachwele – Vancouver Whitecaps, Canada
- Clement Mzize – Young Africans
- Abel Josiah – TDS TFF Academy
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti