Wafungaji Bora Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025

Wafungaji Bora Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025

Mwamba Fiston Kalala Mayele anaandika historia mpya katika soka la Afrika baada ya kutwaa kiatu cha pili cha ufungaji bora kwenye mashindano ya CAF. Awali, Mayele aling’ara akiwa na Yanga SC ya Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAFCC) msimu wa 2023, akimaliza na mabao saba na kutwaa kiatu cha dhahabu.

Lakini mwaka huu 2025, Fiston Mayele ameweka rekodi mpya, akitwaa kiatu cha ufungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) akiwa na Pyramids FC ya Misri.

Mshambuliaji huyo raia wa DR Congo alifunga jumla ya mabao 9, huku goli lake la sita katika hatua ya makundi na mtoano likiwa la ushindi kwenye fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns, na kuiwezesha Pyramids kutwaa taji lao la kwanza la CAF.

Wafungaji Bora Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025

Orodha ya Wafungaji Bora Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025

Nafasi Mchezaji Klabu Mabao
1 Fiston Mayele Pyramids FC 9
2 Ibrahim Adel Pyramids FC 6
3 Imam Ashour Al Ahly 4
4 Lucas Ribeiro Costa Mamelodi Sundowns 4
5 Peter Shalulile Mamelodi Sundowns 3

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fiston Mayele Ndie Mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2024/2025
  2. Washindi Tuzo Za Baraza La Michezo Tanzania BMT 2024
  3. Pyramids Yabeba Ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika 2024/2025 kwa Mara ya Kwanza Kihistoria
  4. Wachezaji wa Simba Walioitwa Kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa June 2025
  5. Hawa Apa Maofisa wa Mechi ya Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
  6. Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa kambini Kuelekea COSAFA na Mechi ya Kirafiki
  7. Coastal Union Yapiga Hesabu Kali Kumchukua Anicet Kiazayidi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo