Singida Black Stars Yawinda Sahihi ya Zawadi Mauya
Zawadi Mauya, kiungo mkabaji wa mabingwa wa ligi kuu ya NBC Tanzania Yanga Sc, anakaribia kumaliza mkataba wake na klabu ya Yanga SC, na Singida Black Stars ipo katika hatua za mwisho za kunasa sahihi ya mchezaji huyo.
Mauya aliwasili Yanga mwezi Julai 2020 akitokea Kagera Sugar FC. Katika kikosi cha sasa cha Yanga, yeye ni mchezaji aliyecheza kwa muda mrefu zaidi.
“Yanga ni klabu yenye mipango mikubwa. Kama mchezaji, nimejifunza mengi na kupata uzoefu kutoka kwa makocha mbalimbali,” alisema Mauya.
“Kucheza na wachezaji wa ndani na wa kigeni kumenifunza mengi katika majukumu yangu. Ninaamini kile ninachofanya ni tofauti na jinsi wanavyoniangalia wengine,” aliongeza.
“Klabu ya Yanga imeacha kumbukumbu nzuri moyoni mwangu. Sikumbuki moja baada ya nyingine, lakini msimu uliopita sikupata nafasi nyingi ya kucheza. Hata hivyo, ilikuwa furaha kubwa kwa klabu yangu kushinda mataji yote muhimu.”
“Ndoto zangu za kushinda mataji na Yanga SC zimetimia,” alihitimisha Zawadi Mauya.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Wachezaji Wapya Azam 2024/2025 (Wachezaji Waliosajiliwa Azam FC)
- Azam Yatuma Ofa Kwa Simba Kumsajili Kipa Aishi Manula
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
- FIFA Yaiondolea Yanga Adhabu ya Kufungiwa Kusajili
- Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025
- Dirisha la Usajili Ligi Kuu Tanzania kufunguliwa Juni 15 hadi Agosti 15, 2024
- Tetesi za Usajili Yanga: Okrah Kwenye Rada za Kuondoka Yanga? Habari Kamili
- Tetesi za Usajili Real Madrid 2024/2025
Weka Komenti